Yafuatayo ni maneno kwenye mistari tofauti iliyoandikwa na Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni miezi mitatu tu imebaki Tanzania kuingia kwenye uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge.
Hii ni tweet ya kwanza aliandika July 4 2015 >>> ‘Utaratibu bora wa kuchagua kiongozi wa nchi si wa kuanza kujadili majina, bali wa kuanza kujadili changamoto na vipaumbele vya Taifa kwanza‘
Tweet alizoandika July 5 2015 >>> ‘Tusiwasikilize wanasiasa wanaowagawa Watanzania na kutumia fedha kutafuta madaraka. Mchezo wao ni mauti yetu. Wakatalieni kwa macho makavu, Tusiruhusu wanasiasa kutumia dini ambazo ni mhimili muhimu wa amani yetu. Ukiwepo mfarakano wa kidini hakuna mtu wala eneo litakalonusurika’
Mstari mwingine ameandika >>> ‘Tukiamua kwa utashi wetu kuzipoteza tunu za amani na upendo, katu hatuwezi kusema ni mapenzi ya Mungu bali itakuwa ni makosa yetu wenyewe, kiongozi wa dini anapaswa kukumbusha wajibu wa: kujiandikisha, kupiga kura na kuchagua kiongozi bora; si kuwaambia waumini wamchague fulani‘