KAMANDA WA POLISI DODOMA AKANUSHA UVUMI WA KUFARIKI DUNIA JOSEPH ELIAZA CHILONGANI ANAYEDAIWA KUPIGWA NA MH. JOB NDUGAI


Mnamo tarehe 28.7.2015 majira ya jioni JOSEPH ELIAZA CHILONGANI alifika katika kituo cha Polisi Kibaigwa akilalalmika kuwa wakati wakiwa kwenye kampeni za kujinadi kwa wanachama kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea ubunge kupitia CCM alishambuliwa kwa fimbo sehemu za kichwani na tumboni na JOB YUSTOO NDUGAI (MB).


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamiz wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema mtu huyo aliyejeruhiwa alipewa PF3 na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa uchaguzi wa madaktari na matibabu. Amelazwa na anaendelea na matibabu hadi sasa, hali yake anaendelea vizuri. 

Kamanda MISIME amesema uchunguzi wa malalamiko hayo unafanyiwa kazi kwa kupata maelezo ya watu walio kuwa kwenye mkutano huo wa kampeni na ukikamilishwa jalada litapelekwa kwa Wakili wa Serikali kwa hatua zaidi za kisheria.

Na. Lakia Ndwellah wa Jeshi la Polisi Dodoma.