Zaidi ya shule 700 Korea Kusini zimefungwa kuhofia kuenea kwa ugonjwa uliozuka kwa ugonjwa unaoshambulia mfumo wa upumuaji uliozuka kutoka Mashariki ya kati wa MERS
Watu watatu hadi sasa wanadaiwa kufa kutokana na ugonjwa huo ambapo pia watu wengine 35 wamebainika kuwa na maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo. MERS ni mara ya kwanza kugunduliwa nje ya Saudi Arabia, kwani miaka mitatu iliyopita mgonjwa wa kwanza aligunduliwa huko Mashariki ya Kati. Rais wa Korea Kusini Park Geun-Hye amehimiza jitihada zaidi kukabiliana na ueneaji wa virusi vya ugonjwa huo. Raia wa Korea kwa sasa wamekumbwa na wasiwasi kutokana na ugonjwa huo wa SARS ulioua mamia ya watu huko Kaskazini Mashariki mwa Asia zaidi ya muongo mmoja uliopita.