IMEDAIWA
kuwa kufungwa kwa wafanyabiashara wanatumia meseji za kufunga maduka huku
wengine wakiwa hawaambiwi sababu ya kufunga maduka na kuwa wengine hawajaona
umuhumu wa kufunga maduka.
Mkoa wa Njombe
karibu wilaya zote maduka ya mijini yamefungwa huku maduka ya pembezoni yakiwa
wazi, na watu kutoka katika maeneo mbalimbali wakikosa huduma na kuwa kufungwa
huko kutadumu kwa siku tatu ambapo wafanyabiashara wanadai kuwa mahakamani
kusikiliza kesi ya Mfanyabiashara mwenzao Jonson Minja inayo sikilizwa mjini
Dodoma.
Akizungumza na
NIPASHE Mkoani Njombe mwenyekiti wa wafanyabiashara na viwanda (TCCIA) mkoa wa Njombe
Menard Mlyuka, alisema kufungwa kwa maduka kutakuwa na madhara yatakayo wapata
wafanyabiashara ambayo ni kupoteza wateja kwa siku hizo tatu.
“Wafanyabiashara
watapata madhara ya kupoteza wateja kwa siku tatu na wateja wao watapata
madhara ya kuto pata huduma lakini kwa Mfanyabiashara ni madhara makubwa kwa
kuwa watahiutaji kulipa mfanyakazi ambaye hajafanya kazi kwa siku tatu na pesa za
matumini kwa siku hizo ambazo atakuwa hajaingiza pesa,” alisema Mlyuka.
Alisema kuwa
kuwapo kwa kufunga funga maduka pia kunamadhara kitaifa katika mfumo wa
biashara ambapo wafanyabiashara kutoka nchi za nje ambao wanajua wanakuja
kupata huduma hapa nchini wanakosa watahama eneo ya kuchukuliwa bidhaa.
“Kufungwa kufungwa
kwa maduka kama soko la Kariakoo wafanyabiashara kutoka Kongo ambao walitarajia
kupata bidhaa wanakuta maduka yamefungwa wanakata tama ya kuja kuchukua bidhaa
hapa nchini na kwenda nje ya nchi kuchukua bidhaa wataangalia ni nchi gali
hakufungwi maduka wataenda kuchukua mizigo huko,” aliongeza
Alisema kuwa
kunawatu wanafunga maduka hata maana ya kufungwa kwa maduka hawajui kwa kuwa
wanatumia tu meseji za kufunga maduka na kuwa viongozi hawajatia elimu ya
kutosha kuhusiana ana kufungwa kwa maduka.
Aidha Mlyuka
alisema kuwa haipendezi kufunga maduka kwa sababu watu hawajapata elimu ya
kwanini wanafunga maduka na kuongeza kuwa kunamaeneo ambako jumuiya ya
wafanyabiashara haijadfika maduka hajajafungwa kama Kigoma, Lindi na maeneo
mengine.