Karibu mwezi Mtukufu wa Ramadhani



Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ni Mwezi ambao inapatikana ibada ya Funga ambayo ni Moja katika Nguzo Tano za Uislamu.

Kwa uwezo wake M/Mungu kwa Mujibu wa Muandamo(Muonekano) wa Mwezi , Tarehe 19/6/2015 ya Mwaka huu huenda tukaanza Kufunga .

JEE? Vipi tunatakiwa Tuu karibishe Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani ?

1.Tusafishe Nafsi zetu  na kila aina ya mabaya.

2.Tuwekee maazimio ya kutorejea tena katika Mabaya tuliyo yafanya .

3.Tusameheane makosa ya kibinaadamu yaliyo jitokeza kati yetu ili tuingie katika Mwezi huu tukiwa mbali na chuki , Magomvi au aina yoyote ya Sinto fahamu kati yetu na hali hii ya UPENDO , iendelee HATA BAADA YA RAMADHANI.

4.Tuombe saana Dua Kwa M/Mungu atubariki kwa masiku yaliyo baki MweZi wa Shaaban na atufikishe Mwezi Mtufuku wa Ramadhani tukiwa  na Afya Njema na uwezo wa kutekeleza Ibada hii ya Funga.  

5. Panga Ratiba yako Mapema ndani yake tenga nafasi ya Kusoma Qur an , kusikiliza Darsa za ki elimu . N.k .

6.TUMUOMBE SAANA M/Mungu kwa barka ya Miezi hii mitukufu ajaalie Nchi yetu amani , Uchaguzi upite kwa Salama na Amani na Tuumpate Kiongozi bora , MZuri , Mwema na M/Mungu asitupe tofauti na  maombi yetu ili upatikane utulivu katika Nafsi , Mioyo ya Wa Tanzania.

IBADA INA HITAJI UTULIVU , BILA YA UTULIVU NA AMANI , TUTAFUNGA KWA SHAKA NA TUTASWALI KWA SHAKA Tumuombe M/Mungu katika kuelekea Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani Nchi yetu ya Tanzania iendelee kuwa na AMANI NA UTULIVU na Nchi Jirani na Dunia nzima kwa Ujumla.

7. Uzoeshe moyo wako na kutoa katika Mambo ya kheri UKIANZIA HILI LA UJENZI WA MSIKITI AMBAO NI NYUMBA YA M/Mungu na imeelezwa katika. hadithi kama alivyosema Mtume (S.A.W) yeyote mwenye kujenga ( kushiriki kujenga Msikiti ) M/Mungu atamjengea Mtu huyo Nyumba peponi ". Hadith

Anza na kheri hii ya Kuchangia ujenzi wa Msikiti huku ukiwa katika maandalizi  ya kuupokea Mwezi huu wenye baraka zaidi kwa kuitakasa nafsi yako na yote tuliyo yatanguliza ili  Tuupate Msamaha , Rehma na Toba ya kweli kwa M/Mungu Mtukufu.