LEO KATIKA HISTORIA: Aprili 28



1923: Uwanja wa Wembley wafunguliwa
Uwanja wa Wembley
Uwanja wa Soka wa Wembley ambao umejichotea umaarufu kwa mechi za Kombe la FA, Michuano ya Olimpiki mwaka 1948, 2012, Fainali za Kombe la Dunia mwaka 1966, Kombe la Dunia la Rugby mwaka 1995, na Fainali za Euro 1996 ulifunguliwa rasmi kwa mechi ya soka katika Kombe la FA; West Ham United kuvutana shati na Bolton Wanderers. 

Hapo awali ulikuwa ukijiulikana kwa jina la ‘Empire Stadium’. Umekuwa ukifanyiwa marekebisho mbalimbali kwa miaka tofauti lakini Mei 20, 2000 kulichezwa mechi ya mwisho ya fainali ya Kombe la FA katika dimba la zamani la Wembley kukishuhudiwa Chelsea ikiitungua Aston Villa kwa bao pekee la Roberto Di Matteo.