MRAJISI wa vyama vya ushirika Tanzania Dkt,
Audax Lutabazibwa amewataka viongozi wa vyama vikuu ya ushirika hapa nchini
kutekeleza mabadiliko ya sheria mpya ya vyama hivyo.
Sheria
mpya ya vyama vikuu ya ushirika ina weka mbali siasa na viongozi wake ili
kufanya utendaji wake kuwa madhubuni na kuwa seria hiyo hairuhusu kiongozi
kujihusisha na siasa.
Akizungumza
kwa niaba ya mrajisi mkuu huyo katika
mkutano mkuu wa vyama vya ushirika mkoa wa Njombe (Njurecu) Mrajisi msaidizi wa
chama kuku cha ushirika mkia wa Iringa, John Kiteve alisema kuwa kuna sheria
imeunda ili kudhibiti viongozi wa vyama hivyo kujihusisha na siasa ili kuepusha
mkanganyiko ndani ya vyama hivyo katika utendaji.
Kiteve
alisema kuwa hali hiyo imelenga kutenganisha miingiliano ya kiutendaji na siasa
wakati wa kutekeleza majukumu ya chama na kuwa wanachama wa kawaida hawazuiwi
kuwa wanasiasa.
Hiyo
aliwataka wanachama wanao taka kugombea katika nafasi yoyote ile katika vyama
hiyo kuhakikisha kuw hawajihusisi na siasa ili kwenda sawa na sheria hiyo na
kuwa kaka kiongozi akigombea na kubainika anajihusisha na siasa atapokwa nafasi
yake.
Akisoma
taarifa ya ushirika huo mwenyekiti wa chama hicho ambaye alikuwa kiongozi na
kuchaguliwa tena kwa awamu nyingine, Clemence Malekela alisema kuwa licha ya
uchanga wa chama hicho kimefanikiwa kupiga hatua kubwa katika kukuza kwa
kuwafikia wanachama na kuwapa elimu juu ya umuhimu chama hicho.
![]() |
Mwenyekiti aliyekuwa akitetea kiti na kushinda Clemence Malecela |
Malekela
alisema pamoja na mafanikio ya kupata soko
la mahindi kwaajili ya wakulima lakini serikali imewakwamisha wakulima
hao kwa kuchelewa
kuwa lipa wa kilima fedha
zao za mazao.
Hata
hivyo chama hicho kimefanya uchaguzi ili kuwapata viongozi wapya kwa sasa ambao
watafanyakazi ya kuendele zaushirika huo.
Katika
uchanguzi huo viongozi walichaguliwa na mwenyekiti wao wa msimu wa kwanza na
wajumbe watatu kuongezwa katika bodi ya uongozi kutoka sita hadi tisa bodi hiyo
ya uongozi wa chama kikuu cha ushirika mkoa wa Njombe.