LICHA ya serikali ya Tanzania kuwa na sera ya kuwa na
zahanati kila Kijiji na kituo cha afya kila kata lakini baadhi ya vijiji na kata hapa nchini bado
vinakabiliwa na changamoto ya kukosa huduma mhimu za afya.
Kijiji cha Mwilamba kata ya Kipengele halmashauri ya wilaya
ya Wanging'ombe ni miongoni mwa wahanga wa kukosa huduma mhimu ya afya kwa binadamu
pamoja na kata nzima ya Kipengele ambayo
ina Zahanati ya kanisa katoliki Pekee na iko mbali na vijiji vingine katika
kata hiyo
Wakiwa katika mkutano wa hadhara mbele ya mbunge wao na
Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge wananchi hao juzi, waliomba suala hilo
lipatiwe ufumbuzi haraka kwa kuwa wameonyesha jitiha kwa kujenga zahanati ambayo
hata hivyo bado haijakamilika.
Johua Mahenge kwa niaba ya wananchi alisema kuwa wanaomba
kukamilishiwa Zahanati hiyo ambayo wameonyesha uzezo kwa kuanza ujenzi kwake
ili waanze kupata huduma jirani.
Alisema wamekuwa wakipata tabu kufuata huduma hizo mbali na
makazi yao hasa wanapo ugua.
Wananchi hao walimlilia mbunge wao juu ya kukosa barabara
na madaraja mhimu ya kuwafikisha katika zahanati ya kipengele kilometa 22 kwa
kuwa ni muda mrefu wameomba bila mafanikio pamoja na kuwa na hofu ya kuuza
mazao yao kutokana na ubovu wa barabara na madaraja
Akisoma taarifa ya kijiji Mwilmba Jordani Mtewele alisisitiza
umhimu wa serikali kufumbua macho yake na kuangazia changamoto za vijiji vyake
na hasa maeneo yanayo sahaulika kama kijiji hicho.
Baada ya kusikia vilio vya wananchi hao Naibu Waziri Ujenzi
na mbunge wa Njombe Magharibi Gerson Lwenge aliamua kuchangia ukamilishaji wa
zahani kijijini hapo kwa kuchangia Bati 150 ili kukamilisha zahanati ambayo
itakuwa mkombozi kijijini hapo
Mbunge huyo pia alitembelea katika kijiji cha Ukomoro kata
ya Kipengele ambako amechangia kiasi cha
shilingi milioni mbili kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mganga.