DAFTARI LAENDELEA NJOMBE



DAFTARI la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR katika  halmashauri ya Njombe, limeendelea vizuri huku walio tumika katika kata za awali kutumika katika kata wanazo zianza leo na kesho katika halmashauri hizoili kukabiliana na changamoto za utumiaji wa mashine hizo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na NIPASHE mkoani Njombe maofisa uchaguzi wasaidisi wa halmashauri za mkoa huo wamesema kuwa watawatumia waandikishaji waliowatumia katika kata walizo anzanazo ili kuhakikisha changamoto za utumiaji wa mashine kuto jitokeza.

Ofisa uchaguzi msaidizi wa halmashauri ya Makete Gregory Emmanuel alisema kuwa katika halmashauri yake wamefanikiwa kuandikisha watu wengi kupita makadilio yao na kufikia asilimia 139 ambapo walitarajia kuwaandikisha watu 10859 na kuwaandikishwa watu 15142.

Alisema kuwa kufikia juzi majira ya jioni watu katika vituo vingine vilikuwa havina watu waliokuwa katika vituo na vituo vingine kulikuw ana watu watano kufikia majira ya saa 11:00 na wanauhakika kuwa watu watu wameandikishwa.

Alisem akuwa ili kukabiliana na matatizo ya matumizi ya mashine na kazi ya utumiaji wake wamejipangakuwatumia watu walewale walio kuwa wamewatumia katika kata walizo anzanazo ili kuto kuwa na ugeni katika katumizi ya mashine na anaimani yakuwa kutakuw na changamoto chache tofauti na awali.

Aliongeza kuwa zoezi hilo katika kata zingine wanatarajia kuanza jumatano huku siku ya jana na leo wakifanya matengizizo na kufanya usafirishaji ili kuhakikisha kwa kata wanazo anzanazo wanaanza kwa pamoja na mashine zikiwa salama.


Kwa upandewake Ofisa uchaguzi msaidizi wa halmashauri ya Ludewa, Gervas Lupembe alisem akuwa katika halmashauri yake wamefanikiwa kumaliza kata 6 kati ya kata 25 za halmashauri hiyo na kuwa kata moja jana wangeimalizia kutokana na kata hiyo kuanza kwa kuchelewa kutokana na vifaa kufika kwa kuchelewa.

Alisema kuwa katika kata zake sita walizo anzanazo na kuwa hakuna kata waliyoongeza muda kutokana na watu kujitokeza kwa wakati na kumaliza siku ya juzi ambayo zilikuwa zinatimia siku saba.

Naye afisa uchaguzi halmashauri ya Wanging’ombe, Christopher Mashaka alisem akuwa katika kata zao walizo anzanazo nne wamefanikiwa kuwaandikishwa watu wote na kuwa  waendelea na kata 5 na kuwatumia waandikishaji walewale walio anzania na kuwa wataongeza wachache kutoka 108 na kuwa 114 ili zoezi hilo kwenda vizuri.

Alisema kuwa wanaimani kuwa zoezi hilo kwa halmashauri hiyo wanauhakika kwenda viruri kwa kuwa wamejipanga kuzifanyia marekebisho mashine ili kutokumbana na mashine kukwamakwama na kuwa changamoto za mwanzo huenda sisijitokeze.

Aidha kwa halmashauri ya Njombe mjini zoezi hilo limeendelea vizuri na kuwa kwa siku ya jana ndio wanamalizia kwa vituo vilivyo kuwa vina watu wengi na kubakia, ambapo waliwaandika majina na kumalizia hiyo jana.

Alisema kuwa kwa siku ya jana kwa baadhi ya vituo walikuwa na watu waliobaki juzi na kuwa kuna vituo havikuwa na watu waliobaki na siku ya leo kuaza katika kata zingine huku siku ya jana wakifana marekebisho na kuwa watatumia waandikishaji walewale katika kata hizo ili kuwa na kasi wakati wa uandikishaji.

Kwa halmashauri ya wilaya Njombe  Dominick Manyenyi alisema kuwa katika halmashauri hiyo zoezi limeendelea vizuri licha ya baadhi ya kata kuanza kwa kuchelewa kutokana na kuwapo kwa changamoto za miundombinu na kuwa kwa kata zinazo fuata watajitahidi siku ya Leo kuhakikisha mashine zinafika kwaajili ya kuaza huku siku ya jana wakifanya usafirishaji na marekebisho.