Na Furaha Eliab, Njombe
MKUU wa mkoa wa Njombe Dtk. Rehema Nchimbi amewataka wakurugenzi
wa halmashauri,wakuu wa Wilaya pamoja na
maafisa Mkoani hapo watakaofanyakazi ya kuwaandikisha wananchi kwenye daftari
la kudumu la wapiga kura kusimamia vizuri zoezi hilo litakapoanza.
Dkt Nchimbi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na vyombo
vya habari pamoja na baadhi ya wazee na viongozi wa dini mkoani hapa juu ya
tarehe rasmi ya kuanza kwa zoezi hilo hapo Februari 23 mwaka huu baada ya
kuahilishwa Februari 16.
“Wakurugenzi, watendaji na mtakao husika katika zoezi hili
mlifanye kwa ufanisi na mhakikishe linafanyika bili kupata dosali mpaka
linanalizika, ili tuonyeshe upendeleo huu kuwa haujakosea kuja katika mkoa wetu
huu,” alisema Dkt. Nchimbi.
Alisema kwa kuwa mkoa wa Njombe umekuwa wa kwanza katika
zoezi hilo muhimu la kitaifa hivyo ni vyema viongozi hao kwa nafasi yao
wakatumia vizuri fursa hiyo kutoa elimu kwa wananchi na waumini wao.
Aidha aliwataka wananchi kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi
kujiandikisha katika daftari hilo la kudumu kwani bila kujiandikisha katika
taftari hilo hawatakuwa na haki ya kupiga kura katika Kura ya maoni ya Katiba
Pendekezwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu.
Aidha Dkt. Nchimbi alisema zoezi hilo litaanzia ndani ya
wilaya ya Njombe katika halmashauri ya mji wa Makambako hivyo ni vyema kila mmoja akashiriki kikamilifu katika zoezi
hilo vikiwemo vyama vya siasa.
“Zoezi hili linalo tarajiwa kuanza Februari 23 mwaka huu
katika mkoa wetu huu litaanza katika halmashauri ya mji mdogo wa Makambako
katika wilaya ya Njombe, kuhusi vifaa na vitu vingine tutawajuza kupitia vyombo
vya habari na msiwe na wasiwasi kuhusu hilo,” alisema Dkt. Nnchimbi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba alisema
atasimamia vizuri zoezi hilo katika wilaya yake pasipo kigugumizi chochote huku
akiwaonya watu watakaoanza kupotosha umma juu ya zoezi hilo.
Nao wadau walio hudhulia katika mkutano huo wa mkuu wa mkoa
walisema kuwa kuhusu vifaa wananchi wasiwe na wasiwasi na uvumi kuwa ni
vichache kwa kuwa zoezi lenyewe bado halijaanza na kuwa wasuburi zoezi lianze
ndipo zianza kutolewa lawama.
Mchungaji Alfred Mwagike wa Tanzania Assemblies of God
(TAG), ni moja ya walio pata nafasi ya kuhuzuria zoezi hilo na aliwataka
wananchi kuacha na uvumi wa kuwa zoezi hilo litagubikwa na uchache wa vifaa
hivyo wajitokeze katika zoeli hilo bila kusitasita na wajiandikishe ili wapate
sifa ya kupiga kura na kupata kitambulisho ambacho kimekuwa kikitumika katika
shughuli mbalimbali.