Akizungumza na gazeti hili eneo la tukio Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kipunguni A, Praxeda Mkandara alisema kuwa alipata taarifa saa 12:00 asubuhi kuwa kuna nyumba imeungua moto na kuteketeza kila kitu na kusababisha vifo vya watu sita.i=ar es Salaam. “Yesu tuokoe, Yesu tuokoe”. Ndiyo sauti ya mwisho iliyosikia toka kwenye nyumba ya vyumba vitatu na sebule iliyoteketea kwa moto na kusababisha watu sita wa familia moja kupoteza maisha, huku miili ya baba na mama wa familia hiyo ikikutwa pamoja imekumbatiana, ikiwa ni ishara ya kufa pamoja.Kila aliyekuwepo kwenye eneo la tukio alikuwa ni mwenye simanzi, hasa waumini wenzake wa Kikristo kwakuwa jana (Jumamosi) ilikuwa ni zamu ya familia hiyo kuwa wenyeji wa sala ya pamoja ya wanajumuiya nyumbani hapo. Moto huo unaosadikiwa kusababishwa na hitilafu ya umeme, ulitokea saa nane usiku katika eneo la Kipunguni A, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Godfrey Mwandosya ni kaka wa marehemu Selina Mpira ambaye ni mke wa David Mpira baba wa familia hiyo, aliwataja watu waliofariki dunia kwenye ajali hiyo ya moto kuwa ni dada yake Selina Mpira, mumewe David Mpira (waliokutwa wamekufa pamoja wakiwa wamekumbatiana), mtoto wao wa kwanza Lucas Mpira, mdogo wake aliyekuwa akiishi na dada yake Samwel Mayegela na wajukuu Selina na Paulina ambao ni watoto wa Emmanuel aliyenusurika baada ya kuwa nje ya nyumba hiyo.
“Tumepanga mazishi yatafanyika Jumanne saa 8:00 mchana katika makaburi ya Airwing Ukonga baada ya kuwasili ndugu wa marehemu waliopo mbali ambao tunatarajia watawasili siku ya Jumatatu,” alisema Mwandosya.
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya waliyokuwa wanasali ambayo marehemu Mpira alikuwa ni Mwenyekiti, Deus Mathias alisema kuwa alifika mahali hapo kwa ajili ya kusali Jumuiya , lakini akiwa njiani akaona moshi na watu wamejaa eneo hilo baada ya kusogea ndiyo akafahamishwa kuwa familia hiyo imeteketea kwa moto.
“Nilifahamishwa kuwa jana usiku walitizama mpira na kulala usiku mkubwa ndiyo maana tukio hilo lilipotokea hawakustuka mapema, lakini waliofika mapema wanasema kuwa walimsikia mwanamke akisema ‘Yesu tuokoe, Yesu tuokoe’ huku mwanaume akiunguruma, lakini ilikuwa ngumu kuwaokoa kwa sababu milango ilikuwa migumu kufunguka na moshi ulikuwa umetanda sana, ”alisema Mathias.
Kwa upande wa jirani wa familia hiyo Mohamed Mwagila alisema kuwa alipata taarifa saa 11:17 asubuhi na alipofika eneo la tukio alikuta tayari watu wamekusanyika na wakajaribu kuvunja dirisha la nyumba hiyo la nyuma ili wawaokoe lakini hawakuona mtu.
Alisema walijaribu kumwaga maji lakini hawakufanikiwa kwa sababu hayakuwapo ya kutosha, hadi Polisi walipofika saa 11:00 jioni na Tanesco walipoachanisha nyaya zinazoleta umeme katika nyumba hiyo, “Polisi wakazikuta maiti tatu ya mjomba na watoto wa dada yake chumba kimoja, ya kijana wao mkubwa chumbani kwake huku ya baba na mama zikiwa pamoja zimekumbatiana, ”alisema Mwagila.
Akizungumza na gazeti hili eneo la tukio Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kipunguni A, Praxeda Mkandara alisema kuwa alipata taarifa saa 12:00 asubuhi kuwa kuna nyumba imeungua moto na kuteketeza kila kitu na kusababisha vifo vya watu sita.
Mkandara alisema katika nyumba hiyo wanaishi watu saba, lakini mmoja aliyemtaja kwa jina la Emmanuel Kirigiti inasemekana alikuwa Java kwenye muziki, wakati tukio hilo linatokea hakuwapo ndani na ndiyo manusura yake.
Akizungumza katikia eneo la tukio Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Jerry Silaa alisema kwa sababu waliokufa ni wanafamilia hivyo wao kama Serikali watalibeba jukumu hilo hadi siku ya Jumanne yatakapofanyika mazishi.
Alisema alikuta Polisi na Zimamoto wamefika na kutoa miili ya marehemu, walipotaka kuondoka jirani mmoja akasema ndani ya nyumba hiyo wanaishi watu sita mbona miili imetoka mitano, hivyo Polisi wakalazimika kurudi ndani na kupekua na kupata mwili mwingine.