CHAMA cha mapinduzi (CCM) kinawasiwasi na kasi ya elimu na usambazaji
wa Katiba Pendekezwa (KP) kama itawafikia wananchi wote kulingana na uchache wake
na muda uliobakia.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara
yake ya siku tatu mafunzo mkoani Njombe, Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Philip Mangula, alisema kuwa
anawasiwasi na kasi ya usambazaji wa KP kuwa kama itawafikia wananchi wengi
mpaka kufikia muda wa kuipigia kura wakati kumebakiwa na miezi miwili kuipigia
kura kutokana na mfumo unaotumika na
uchache wake.
Magula alisema kuwa kasi inayotumika kusambaza ni ndogo na
kuwa amepita sehemu nyingi hapa nchini ambapo katika ziara hiyo mpaka sasa ni
mikoa 21 amepita na sehemu nyingi haijafika na wananchi wanadai hawajaiona na
wanahamu ya kuiona.
Alisema kuwa mfumo unao tumiwa kutoa elimu mpaka sasa ni
mfumo unao walenga watu wachache na hasa matajiri na wenye hali ya kati kwa
kuwa zinatumika Luninga ambapo ni watu wachache wenye nazo na kuwa hata
walionazo kunawasisi na utazamaji wake.
“Nina wasiwasi kwa mfumo unaotumika kutoa elimu unaoendelea
kama tutawafikia watu wengi zaidi kwa kuwa elimu inatolewa kupitia Terevisheni
ya taifa TBC 1 kuna vipindi huko lakini wapigakura wengi hawana televisheni
watu wachache wanafikiwa na elimu hiyo pia hata katika magazeti watu wa
vijijini wengi hawanunui wala kusoma magazeti,” alisema Mangula.
Alisema kuwa nakala zilizo tolewa nichache kulingana na
mfumo utakao tumika na kama mtu atakaye pewa ataweka nyumbani kwake kama
maktaba lakini kama mtu atakayepewa ataenda kuwaeleza wenzake nakala huenda
zikatosha.
Alisema kuwa katika kila kata itapatiwa nakala 300 za KP na
kuwa muundo wake wa namna ya kusambaza utakuwa ni mzuri kwa kuwa baada ya
kufika katika kata husika na kata itasambaza katika vijiji na hatimaye katika
mtu mmoja mmoja, na kuwa kama itatumika mfumo huu inaweza kufika kwa haraka kwa
wananchi
Aliongeza; “Nakala milioni 2 zinaweza kutosha kama kila
atakayepewa atatoa elimu kwa wenzake, lakini kama atachukua na kuweka nyumbani
kwake hazita tosha kwa sababu zitapotelea kwa watu milioni mbili pekee, lakini
naona mfumo huu wa kusambaza katika kila kata ni mzuri utawafikia wananchi,”
Mangula alitoa ushauri kwa serikali na wanao husika na
usambazaji kuhakikisha nakala zinaongezwa ili kuw ana uhakika wa kufikia
wananchi wote wenyesifa za kuipigia kura na kuisoma kasha uielewa.
Hata hivyo Mangula alisisitiza taasisi zisizo za kiserikali (NGO’s)
zitakazo kuwa zikijihusisha na elimu kwa umma juu ya KP kuwa ni zile za mkoa na
wilaya husika kwa kuwa zinafahamu mazingira na wananchi wanaelewana kwa maneno
ya kutumia wakati wa kutoa elimu.
“Ninatoa ushauri kwa wanaozipitisha NGO’s za kutoa elimu
waangalie inaenda kutoa elimu wapi haiwezekani taasisi kutoka Arusha Ikaja
kutoa elimu huku Njombe kwa kuwa haifahamu ni maneno gani yakitumika wananchi
wataelewa zaidi na manenogani hawata elewa au wanayachukia lakini ikiwa ni
taasisi ya eneo husika itasaidia kuepuka vikwazo kwa wahusika,” alisema
Mangula.