WATU WAWILI WAUWAWA NA WATU WASIYOFAHAMIKA MKOANI NJOMBE

     

Watu Wawili Wamefariki Kwa Kuuwawa Na Watu Wasiyofahamika Katika Matukio Mawili Tofauti Mkaoni Njombe Likiwemo La Mkazi Wa Kijiji Cha  Ufwala  Kata Ya Ilembula Wilayani Wanging'ombe Christopher  Gerevas Maarufu Kwa Jina La Dava  Aliyekutwa Amefariki Kwa Kukatwa Na Kitu Chenye Nja Kali.

Katika Taarifa Ya Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Iliyosainiwa Na Kamanda Wa Jeshi  Hilo SACP Fulgence Ngonyani Imemtaja Christopher Gerevas Maarufu Kwa Jina  La Dava  Mwenye Umri Wa Miaka 32  Mkazi Wa  Kijiji Cha Ufwala  Na Mwili Wake Kukutwa Na Majeraha  Yaliyochomwa Na Kitu Chenye Nja Kali Sehemu Za Kichwani Na Kwenye Jicho Na Kulazwa Kifudifudi Kwenye Mto  Kiwogeka.

 Amesema Kuwa  Pembeni Mwa Mwili  Wa Marehemu Huyo Kumekutwa Na Panga  Ambapo Arifariki Januari 4 Mwaka Huu  Wakati Akichunga Ng'ombe Polini Na Hakuna Ng'ombe Yeyote Aliyeibiwa Katika Tukio Hilo.

Katika Tukio Lingine  Mkazi Wa  Kijiji Cha Image   Kata Ya Kidegembye Joseph Kinyamagoha    Mwenye Umri Wa Miaka 54 Amekutwa Amefariki Dunia Nje Ya Nyumbani Kwake Kwa Kuuwawa Na Watu Wasiyofahamika   Katika  Tukio Lililotokea Januari  2 Mwaka Huu Majira Ya Saa Tano Usiku  Kwa Kukatwa Na Kitu Chenye Nja Kali  Kichwani Na Mkononi.

Kamanda Ngonyani Amesema Chanzo Cha Matukio Hayo  Yote  Bado Kinachunguzwa  Kwa Kushirikiana Na Vikosi Vya Ulinzi Shirikishi  Vya Maeneo Husika Ambako Matukio Hayo Yametokea  Huku Likisema Hakuna Mtu Yeyote Anaeshikiliwa Kuhusika Na Matukio Hayo.