Raia wa Syria wapewa masharti Lebanon


Lebanon imepokea Wakimbizi zaidi ya Wakimbizi milioni moja kutoka nchini Syria
Masharti mapya yamewekwa na mamlaka ya Lebanon kwa Raia wa Syria wanaoingia nchini humo , wakati huu ambapo nchi hiyo inapokea Wakimbizi wengi.
Kwa mara ya kwanza, Raia wa Syria watalazimika kuwa na vielelezo vinavyoeleza kwa nini wanataka kuvuka mpaka na kuingia nchini Lebanon.
Masharti haya mapya yanaanza kutumika siku ya jumatatu.Awali kusafiri kati ya nchi hizo mbili kwa kiasi kikubwa hakukuwa na kikwazo lakini sasa Raia wa Syria lazima wawe na Viza.
Hatua hii inaelezwa kulenga kudhibiti idadi kubwa ya Wakimbizi wanaoingia nchini Lebanon, ambapo kwa sasa Lebanon ina wakimbizi zaidi ya milioni moja.
Hatua hii ya sasa haijulikani italeta athari gani kwa Raia wengi wa Syria walio nchini Lebanon ambao hawajajiandikisha kuwa wakimbizi.
Kabla ya sasa, Raia wa Syria waliweza kukaa nchini Lebanon mpaka miezi sita, lakini sasa raia wa nchi hiyo watalazimika kutimiza vigezo kadhaa ili kupatiwa Viza mpakani.