BAADHI ya wafanyabiashara na wakulima wa zao la viazi mkoani Njombe wamelalamikia ubadhiulifu unaofanywa na kamati ya kuzuia rumbeza, kisha kufukuzwa kwa wateja wao ambao walikuwa wakitegemea kuwapata kwa msimu huu wa viazi.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti na waandishi wa habari mkoani Njombe wafanyabiashara hao wamesema kuwa
wamekuwa wakitozwa fedha zisizo na kiwango maalumu kama faini ya kujaza viaji
katika magunia maarufu kama rumbesa, ambapo wamekuwa wakifanya hivyo kwa lengo
la kushindania soko la zao hilo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wafanyabiashara
wa viazo mkoani Njombe Ephraim Haule alisema kuwa msono ambao unatakiwa
kushonwa katika magunia ya viazi wafanyabiashara wanao jumua viazi hizo kutoka
jijini Dar es Salaam wanakataa kununua viazi hivyo kwa kuwa watashindwa kuviuza
wakifika sokoni.
Alisema kuwa wakulima
wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu wa kufanya biashara hiyo kutokana na
kukimbiwa na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakikamatwa wakiukwapo kushona
mshono unao takiwa wakati wa kujumua viazi.
Alisema kuwa
wafanyabiashara wengi wamekimbilia mikoa ya Mbeya na Arusha ambao viazi hivyo
havina mashariti ya kushona wanapo nunua na hakuna wanapo zuiliwa kuhusiana na
mshono na kuwa wakiingia sokoni wanashindana na walio shina mshono wa bila
rumbesa.
Nae Charles Sanga alisema kuwa wamekuwa
wakikabiliana na kukimbiwa na wateja wafikapo katika soko la viazi kutokana na
viazi vyao vimekuwa katika magunia yaliyo na ujazo mdogo ambapo viazi kutoka
mikoa ya Mbeya Iringa, Arusha na nchini Kenya kuwa na rumbesa.
Alisema kuwa chaajabu
ofisi ya mkuu wa wilaya ya Njombe iliunda tume ambayo inapambana na kuzuia
rumbesa katika vizuizi mbalimbali mkoani hapo na kuwatoza faini wanunuzi ambao
wamejaza viazi kwa kuweka rumbesa na kuwa zoezi hilo lilianza kwa kushitukiza
bila ya kutolewa kwa elimu.
Mmoja wa wafanyabiashara
aliye bahatika kukutanana na tume ya ofisi ya mkuu wa wilaya Kanoti Bosco,
alisema kuwa alitozwa faini ya zaidi shilingi 520,000 na kukatiwa stakabaadhi
ya shilingi 420,000 na kudaiwa kuwa shilingi laki moja ni kwaajili ya mafita ya
kuwafuata huko waliko katika vituo ya
kukagulia magunia.
Alisema tume hiyo iliyo
undwa imekuwa ikisimamisha magali hovyo hovyo pasipo kuwa na vituo maalimu na
kuwa stakabaadhi hizo wanamashaka na zo na fedha hizo zinako pelekwa.
“Katika tume hiyo kuna
watu ambao tulikuwa nao katika biashara na wanatuambia watakukomesha mwaka huu
kwa kututoza faini na mpaka watanufaika kupitia faini wanazo tutoza,” alisema Bosco.
Alisema kuwa serikali
kwa kufanya hivyo inawadidimiza wafanya biashara na wakulima kwa kuwa zao hilo
halitunziki gharani na kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto ya kuhalibikiwa
kwa zao hilo kutokana na kukusa wateja hukulikiwa tayali limesha tayarishwa
kuingia sokoni.
Aidha Patrick Nestoli alisema kuwa tume hiyo imeanzishwa
kwaalili ya kuendeleza rushwa kwakuwa wamekuwa wakifanya maelewano baina ya
wafanya biashara mwenye rumbesa na mkamata rumbesa na kutolewa pesa iliyo chini
ya kiwango cha faini na kuachiwa waendelee na safari.
Alisema kuwa wanao
kamatwa na rumbesa wengi wamekuwa wakikamatwa
na rumbesa na kuachiwa waendelee na rumbesa yao huku wakiwa wametoa
faini kitu ambachio hakita dhibiti tatizo la rumbesa bali kitaongeza suala la
rushwa.
“Serikali kama ing’ekuwa
na lengo la kudhibiti tatizo la rumbesa basi mtu akikamatwa na rumbesa
ang’etakiwa kufumua rumbesa na kushona upya magunia take ya viaza, pia mkulima
ambaye anauza bila rumbesa anauza gunia hadi shilingi 20,000 wakati mkulima akiweka
rumbesa anauza mpaka 60,000 wakati katika rumbesa kiasi kinachopungua ni si
zaidi ya debe moja,” Alisema Nestoli.
Swali je ni kwa jinsi
suala la rumbesa udhibiti wake uanzie wapi shambani ama sokoni, Erasto Kitwika
anafananua mbinu ya kudhibiti zai hilo na kusema kuwa udhibiti wa zao hilo
kuhusu rumbesa uanzie sokoni kwa kuwa hapo ndipo penye ushindani.
Alisema kuwa serikali
iwekeudhibiti katika soko na kuweka faini ambayo kila mfanyabishara anaona ni
hasara kudhidisha rumbesa katika magunia yake ya viazi na kujidhibiti mwenyewe.
Alisema kuwa
wafanyabiashara wao hawana shida na kuto weka rumbesa shida ipo katika
ushindani wa soko ambapo wao wakitoka shamba wanakutana na rumbesa na kuwa
kiazi kunacho toka nchini Kenya kinajazwa nusu ya gunia kama rumbesa na inaitwa
Obama.
Kwa upande wake mkuu wa
wilaya ya Njombe Sarah Dumba alisema kuwa tume hiyo ni yeye ameiunda baada ya
kuona wananchi wanakandamizwa na rumbesa kwakuwa ujazoi huo una kiuka sheria ya
vipimo ambao inatakiwa mazao yoyote ya chakula yanatakiwa kuuzwa yakiwa katika
vipimo vya mizani.
Alisema kuwa tume hiyo
awali ilikuwepo na kudhibiti tatizo hilo la rumbesa kwa mkoa wa Njombe na
lilipotea, tume hiyo imeanza baada ya kuona kuwa suala la rumbesa limelejea
tena.
“Katika msafara wa
mambana kenge wamo malalamiko ya kuwapo kwa ubadhirifu yapo na watakao fanya
ubadhilifu wowote katika tume ya kudhibiti rumbesa atakuwa ni muharufu kama
waharifu wengine hivyo sheria haita muacha nyuma itatukua mkondo wake,” alisema
dumba.
Alisema kuwa katika
msafara wa mamba na kenge wamo kwa maana kuwa huenda kuna rushwa ikawepo katika
tume aliyo iunda ambapo katika tume hiyo kuna mtendaji wa kata husika kilipo
kituo cha ukaguzi na kuwa amewapa vitambulisho ili kutambulika na kujitenga na
wahalifu ambao wanaweza kutumia zoezi hilo vibaya.
Alisema kuwa zoezi hilo
lipo katika wsilaya yake pekee na kuwa yeye anazungumzia kwa eneo analo liweza
hivyo litakuwa ni endelevu na likiwa na lengo la kunufaisha mkulina na
kuyapinga malalamikmo ya wafanyabiashara ya kukosa soko nakuwa kiazi kinacho
toka wilayani Njombe kinasoko kuliko cha kutoka mahali popote Tanzania.
“Adhabu kwa watu
wanaokamatwa na rumbesa ni kurubagi (kushona upya gunia) na faini kwa mhusika
maanayake watu hawa wanawanyonya wananchi wanao hangaika kugharamia molea, na
pembejeo zingine,” aliongeza Dumba.