VIONGOZI wa saccos hapa nchini wametakiwa kutazama kwa
umakini michanganuo ya wanachama wao wanao hitaji mikopo ili kukabiliana na
tatizo la kuwapo kwa watu wanao shindwa kulipa malejesho ya mikopo yao.
Hayo yamebainishw ana mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe mkoani
Njombe wakati wa uzinduzi wa Saccos ya Vijana Ulembwe Saccos limited ya
wilayani humo, amesema kuwa uongozi wa saccos uangalie kwa makini mchanganuo
kwa lengo la kukupisha mtu anayeweza kurejesha mkopo.
Alisema kuwa kumekuwa na matatizo ya kuto rejeshwa kwa
mikopo katika saccos nyingi hapa nchini kutokana na wakopaji kuto kuwa na
michanganuo sahihi wa pesa anayokopa.
Amesema kuwa asilimia kubwa ya wananchi wamekuwa
wakijiingiza katika mikopo kwa kuiga na kujikuta wakibadilisha sehemu za kukopa
kwa kulipa madeni katika saccos za awali.
Kwa upande wake wananchi na viongozi wa Kijiji Cha Ulembwe
ambapo nio makao makuu ya sakosi hiyo wamewataka vijana kujiunga katika vikundi
mbalimbali zikiwemo sakosi ili kuweza kusaidiwa na serikali katika mikopo yake
kwa vijana.
Katibu wa saccos amesema kuwa kupitia hapo wataweza
kuwakopisha vijana hasa zile pesa za serikali zilizo tengwa kwajili ya vijana
na wanawake kwa kuwa hapo ni sehemu ambayo ni salama na inaaminika kama anavyo
eleza.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Ulembwe, Peter Luhasi amewataka
wananchi hao waliojiunga katika sakosi hiyo na kupata mkopo wa pembejeo za
wakati wa uzinduzi wakawe mabarozi wazuri kwa wenzao ili nao wajiunge, huku
diwani wa kata hiyo akipongeza juhudi za wananchi waliojiunga ma saccos hiyo na
kunufaika na matunda ya mikopo.
Aidha mkuu wa chuo cha maendeleo ya jamii Yohanes Chongolo
amehimiza wananchi kujitokeza kujionga ili kuunganisha nguvu katika sakosi kwa
kuwa kwa mwananchi wa sasa bila kupopa hawezi kufanya maendeleo sabidi lakiji
wakiunganisha mitaji yao wataendelea kwa kukopeshana.