Uturuki kupokea misaada zaidi.

 

Mjadala unaendelea hapa na pale.
Umoja wa ulaya utaisaidia Uturuki msaada wenye thamani ya dola za kimarekani milioni themanini,ili kuwasaidia wakimbizi walioko kwenye mgogoro wa kivita kati ya Syria na Uturuki,kwasasa wakimbizi wa Uturuki wamefikia asilimia 1.6 milioni.
Mkuu wa umoja wa ulaya wa misaada na sera za kigeni, Federica Mogherini, ametoa tamko la msaada huo akiwa mjini Ankara,alipokuwa katika ziara ya siku mbili kwa lengo la kukuza ushirikiano katika kuwapiga vita wanamgambo wa dola ya kiislam.
Lakini lengo la pili la ziara yake nchini humo ni kuharakisha nchi ya Uturuki ijiunge na Umoja wa Ulaya,harakati zilizoanzwa mwaka 1987 ni baada ya kuweka sheria za sera za kigeni hivi karibuni na hali ya mahusiano kutetereka.