Baada ya kuolewa mwaka 1998 na kuamua kuachana na mumewe ambaye alikua mwanamuziki Christopher ‘Sixx Nine’ mwaka 2002,mwigizaji nyota Vivica Fox aliingia kwenye skendo za mahusiano ya kimapenzi kwa kutembea na wanaume wenye umri mdogo.
Vivica Fox ambaye jina lake kamili ni Vivica Anjanetta Fox ameendelea kutikisa vyombo mbalimbali vya habari duniani kutokana na kuendelea kuwa na mahusiano na wavulana wadogo ambapo kwa sasa ameripotiwa yupo katika uhusiano na muigizaji mwenzake Robert Ri’chard mwenye miaka31.

Vivica ambaye alizaliwa miaka 50 iliyopita walikutana na migizaji huyo wakati akicheza filamu yake ya Chocolate City ambayo illirekodiwa jijini Lagos Angeles mwezi September ambapo kijana huyo alikua akiigiza kama mwanafunzi wa chuo huku Vivica akiigiza kama mama yake mzazi na kujikuta wakiingia katika ulimwengu wa mapenzi.
Hii si mara ya kwanza kwa nyota huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na vijana walio na umri mdogo kwani mwaka 2003 aliingia kwenye skendo baada ya kutembea na mchezaji Darien McCants mwenye miaka 24 kabla ya mwaka huo huo kutembea na mwanamuziki nyota 50 Cent ambaye kwa kipindi hicho alikua na miaka 27 wakati yeye akiwa na miaka 38.
Mwaka 2008 akiwa na miaka44 alianza mahusiano tena na promota Omar Slimm White na baada ya miaka mitatu ya mahusiano yao waliachana mwaka2011.

Miongoni mwa filamu zilizoweza kumpatia umaarufu mwanamama huyu ni pamoja na Independence Day, Set It Off, Soul Food, Why Do Fools Fall in Love, Kill Bill, Booty Call, Sharknado 2,The Second One na Juwanna Mann.
Vivica Fox ambaye jina lake kamili ni Vivica Anjanetta Fox ameendelea kutikisa vyombo mbalimbali vya habari duniani kutokana na kuendelea kuwa na mahusiano na wavulana wadogo ambapo kwa sasa ameripotiwa yupo katika uhusiano na muigizaji mwenzake Robert Ri’chard mwenye miaka31.
Vivica ambaye alizaliwa miaka 50 iliyopita walikutana na migizaji huyo wakati akicheza filamu yake ya Chocolate City ambayo illirekodiwa jijini Lagos Angeles mwezi September ambapo kijana huyo alikua akiigiza kama mwanafunzi wa chuo huku Vivica akiigiza kama mama yake mzazi na kujikuta wakiingia katika ulimwengu wa mapenzi.
Vivica Fox na Robert Ri’chard wakiigiza filamu yao ya Chocolate City.