Kafulila: Escrow inaingoa CCM
Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila amesema Licha ya Chama cha Mapinduzi CCM kuwadharau Watanzania na kuamini kuwa hawana madhara kwa ustawi wake, kashfa yawizi wa fedha akaunti ya Tegeta Escrow itaking’oa Chama hicho madarakani.
Kauli hiyo imetolewa na Mbuge huyo wakati Rais Jakaya Kikwete akisubiriwa kuchukua hatua kutokana na mapendekezo manane ya Bunge yaliyotolewa na Ripoti ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu ukaguzi wa fedha hizo.
Kafulila alisema licha ya wnanachi kukerwa na tabia ya wizi na ufisadi wa mali za umma,bado CCM imeendelea kuwadharau kwa vile wananchi hao kila mara wanaunga mkono chama hicho.
Alisema nchi ipo njiapanda na hali ni mbaya kwa vile licha ya uchumo kuporwa na watu wachache,Serikali imeshindwa kuwachukulia hatua stahiki wahusika na kuwapeleka mahakamani
By Mwananchi