Serikali imesema hadi sasa inakabiliwa na deni la bilioni140 lililosababishwa na uzembe pamoja na ubadhirifu katika Shirika la ndege la Tanzania ATC.
Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe alisema Serikali inakusudia kulipa deni hilo kwa mkupuo hadi litakapopungua zaidi ili kutoa nafasi ya kuimarisha upya sekta ya usafiri wa anga nchini.
Alisema imefikia wakati sasa Tanzania inapaswa kuwa na Shirika imara la ndege ili kuepuka kurudia uzembe na ubadhirifu uliojitokeza miakaya nyuma ATC.
Alisema Serikali itahakikisha Kila Mtanzania anatumia usafiri wa anga na si matajiri pekee kwa kuwa ipo kwenye mchakato wa kumalizia upanuzi wa viwanja vya ndege ilivyoanza,ikiwemo kujenga viwanja katika Mkoa ambayo hana kama Tanga,Shinyanga,Mara na Ruvuma.
By Mnzalendo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)