WAKULIMA MKOANI IRINGA


Wafanyakazi wa mashambani na kilimo Mkoani Iringa wametakiwa kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao pindi mchakato wa utoaji wa maoni kwenye rasimu ya pili katiba utakapoanza.
Katibu Wa Chama cha Wafanyakazi na kilimo Tanzania (TPAWU) Mkoa wa Iringa Bw.Deusdedith Magesa amesema wafanyakazi kwenye taasisi na mashirika mbalimbali wanakabiliwa na changamoto nyingi hivyo kwa njia ya kushiriki kupiga kura ya ndio au hapana itapelekea kuziondoa changamoto hizo.
Bw.Magesa ameongeza kuwa wafanyakazi hao watumie mda wao mwingi kuisoma rasimu hiyo ya katiba na kuacha kutoa maoni yao kwa shinikizo la makundi ya watu ikiwa ni pamoja na kutomiwa na baadhi ya viongozi wa siasa kwa malengo yao binafsi.
Aidha amewataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo yao binafsi na taifa kwa ujumla na kufuata sheria,taratibu na kanuni pamoja na kudumisha sheria ya mahusiano mahala pa kazi.
Hata hivyo Bw.Magesa ametoa wito kwa wafanyakazi hao kushiriki kwenye mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu kwa kupiga kura ya kuwapata viongozi bora pamoja na kujitokeza kugombea kwenye nafasi mbalimbali za uongozi wa nafasi hizo.

Related Posts