- Waaswa kuto ongozwa na wanasiasa
VIJANA kote nchini
wametakiwa kusoma kwa makini rasimu zote mbili za katiba ili kufanya uchaguzi
sahihi wa ukifika wakati wa kuipigia kula katiba na kuacha kuongozwa na vyama
vya vyama vya siasa.
Akizungunza na vijana katika siku ya Nyerere day mkoani hapa
Mwenyekiti wa Jukwa la Vijanamkoa wa Njombe, Luka Mhaya, alisema kuwa vijana
ili kuchagua rasimu au kuipinga rasimu iliyo pendekezwa ni vema wakapitia kwa
makini kipengele hadi kipengele ili kuhakikisha vitu vyenye maslahi kwao kama
vipo.
Alisema kuwa vijana wamekuwa wavivu wa kusoma na kupelewa
kama bendela fuata upepo na taasisi mbalimbali vikiwemo vyama vya siasa.
“Vijana ili kuhakikisha mnaipitisha Katiba itakayo kuwa ni
mstakabali wa maisha yetu ni vima tukaisoma rasimu hii ka kulinganisha na ile ya
Tume ya mabadiliko yakatiba Chini ya Jaji Warioba ili kufanya uchaguzi sahihi
na kuachana na kusikiliza kutoka vyama vys siasa,” alisema Mgaya.
Alisema kuwa katika rasimu hiyo kama vijana wenyewe wakasoma
na kuona inawafaa ni uamuzi wao au haifai ni uamuzi wako kuliko kama watabaki
wakihangaika na kusikiliza wanasiasa wataweza kuchaguliwa kitu ambacho
hakiwahusu.
“Vijana licha ya kusoma kwa makini Rasimu hizo mbili bali
mjitokeze kujiandikisha katika daftali la kupigia kura ili kupata sifa ya
kupiga kula katika rasimu hiyo,” aliongeza Mgaya
Alisema kuwa vijana hawapashwi kulaumu serikali kwa lolote
linalo fanyika ni kutokana na serikali kukasimisha madaraka na madaraka kupewa
serikali za mitaa na mambo yanayo fanyika ni kutokana na viongozi walio wachagua.
Alisema kuwa ni vema vijana kwa kipindi hiki uchaguzi wa
serikali za mitaa wafanye uchaguzi sahihi katika serikali za mitaa na
kujitokeza kuchukua nafasi za uongozi ili kufanya mabadiliko na kuondokana ulalamikaji
kwa viongozi wasiofaa.