Wasaniiwa muziki wa asili wakitoa burudani katika tamasha la Jambo festival.
Mwenyekitiwa Tamasha la sanaa na utamaduni Arusha maarufu kama JamboFerstival Augustine Michael Namfua
Jiji la Arusha litatikiswa na tamasha la sanaa na utamaduni la
kimataifa maarufu kama Jambo festival litakalojumuisha ngoma za asili,mavazi ya asili ,muziki wa asili,mavazi na vyakula ,tamasha hilo litatikisa viunga vya jiji la Arusha ambalo ni kitovu cha utalii.
Takribani watu 3000 kutoka sehemu mbali mbali nchini na nje ya nchi
wanatarajia kuhudhuria tamasha hilo ambalo hutoa burudani isiyo kifani
na lenye kila aina ya ubunifu .
Wageni kutoka nchi za Afrika Mashariki Kenya,Rwanda,Burundi,Nchi za
Ulaya,Marekani na Asia wanatarajia kuhudhuria huku wenyeji wao wakiwa
ni wakazi wa Arusha.
Mwenyekiti wa Tamasha la Jambo Festival , Augustine Michael Namfua
anaeleza kuwa tamasha hilo limekua likifanyika miaka 2 mfulululizo na
kwa sasa linasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa sanaa na utamaduni.
Augustine anaeleza kuwa kila mwaka wamekuwa wakifanya tamasha hilo
lengo ni kuonyesha kazi za sanaa hususani tamaduni.
Tamasha hili limekua likiwaunganisha kwa pamoja wapenzi wa sanaa na
utamaduni wa Watu wa Arusha,Tanzania na Afrika kwa ujumla hasa
ukizingatia kuwa Arusha ni makao makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki
na ni mji wa utalii.