Watoto
watano katika jimbo la Texas nchini Marwaliokutana na mwanamume
anayeugua Ebola nchini humo, wanachunguzwa kwa karibu nyumbani kubaini
ikiwa wana dalili zozote za ugonjwa huo.
Kwenye mkutano na wandishi wa habari katika hospitali yaTexas Health
Presbyterian mjini Dallas, gavana wa jimbo hilo alisema kuwa wazazi wa
watoto hao wana wasiwasi lakini aliwahakikishia kuwa hakuna tisho la
maambukizi.
Maafisa wamesema kuwa watoto
hao wanachunguzwa kwa karibu na nkwamba kuna wanawachunguza watu wengine
12 au zaidi ambao huenda walikaribiana na mwanamume anayeugua Ebola.
Mgonjwa huyo ThomasDuncan anaaminika kuambukizwa Ebola alipokuwa nchini Liberia. Raia huyo wa Liberia aliingia
nchini Marekani wiki mbili zilizopita kuwatembelea jamaa wake, na ni mtu
wa kwanza kugunduliwa na Ebola akiwa nchini Marekani.
Bwana Duncan yuko katika hali mbaya kwa mujibu wa wahudum,u wa afya wanamuhudumia. Muuguzi alimuuliza bwana Duncan
alipotembelea hospitali lini alianza kujihisi mgonjwa na ikiwaaliwahi
kuwepo katika eneo lililoathirika na Ebola.
Alimwambia kuwa
alikuwa ametembelea Liberia, lakini taarifa aliyokuwa anatoa hakuwa
ameitoa kwa kikosi kizima kilichohusika na matibabu yake hospitalini.