Ripoti
ya Kamati ya Mifugo,Utalii, Uwezeshaji na Habari imeitaka Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kuipitia upya mikataba ya Ujenzi wa Miundombinu na
Uendeshaji wa mitambo ya Digital kati ya Wizara ya Habari Utamaduni
Utalii na Michezo na Kampuni ya AGAPE.
Akiwasilisha Muhtasari wa Ripoti ya Kamatihiyo
katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani, Mwenyekiti wa Kamati
hiyo Mlinde Mbarouk Juma amesema kumekuwa na malalamiko mengi na shutuma
mbali mbali kutoka kwa makundi tofauti ya jamii kuhusiana na mradi
huo hivyo Kamati haikuridhishwa na utendaji wa Kampuni hiyo.
Amesema
kuwa Wawekezaji wa AGAPE wameshindwa kufanya kazi na kuitia hasara
serikali kwa kutumia wataalamu na rasilimali za serikali na hatimae
kushindwa kukidhi mahitaji wa wananchi.
Aidha
Kamati imesikitishwa sana na mikataba ya usimamizi na uendeshaji kati
ya Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo na wawekeza wa AGAPE
kwamba haufahamiki vizuri katika utendaji wake.
“Kamati
imegundua kwamba Shirika la Utangazaji Zanzibar halikushirikishwa
kikamilifu katika maamuzi wala mapato yanaypatikana katika mradi huo wa
Digital”, alifahamisha Mwenyekiti huyo.
Kamati
hiyo pia imesikitishwa na matumizi mabaya ya Jengo la zamani la ZBC
ambalo limebadilishwa na kufanywa kuwa nyumba ya starehe kinyume na
matumizi yake ambalo hukodishwa na kufanyiwa shughuli mbali mbali za
kijamii zikwemo harusi na siku ya kuzaliwa (birth day)na kupoteza haiba
yake.
Hata
hivyo Kamati hiyo imeshitushwa na taarifa za uvamizi uanoendelea katika
shamba la Mifugo Pangeni katika Mkoa wa Kaskazini Unguja na kusema kuwa
vitendo hivyo vimeshamiri katika maeneo mbali mbali ambavyo huleta
hasara kwa serikali.
Akichangia
Ripoti ya Kamati hito Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Ali
(Jazira) ameomba serikali kuwapatia maposho yao kwa wakati waandishi wa
Habari wanaohudhuria katika kikao cha Baraza la Wawakilishi .
Mwakilishi
huyo amefahamisha kuwa waandishi wa habari wamekuwa hawapatiwi posho
zao kwa wakati kitendo ambacho kinawavuja moyo na kufanya hivyo ni
kutowafanyia haki na mshahara wao pia mdogo sana ukilinganisha na kazi
wanazozifanya.
Na Miza Kona Maelezo Zanzibar