Wananchi wakiangalia lori baada ya kuungua.
LORI la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida na kuua watu wanne hapohapo.
Chanzo cha
ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa
linashuka mlima huo.Shuhda wa ajali hiyo bwana Julius chacha alipoongea
na mtandao wetu wa Elimtaa blog amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia
lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
Akiendelea
kuongea shuhda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa
moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.
Watu
wanne wamekuufa papo hapo kutokana na ajali hiyo.
Polisi walikuwa bado
hawajafika eneoo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.
Mabaki ya lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii.
Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililoungua jioni hii.
Bonde la mlima Sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeungua.
Hii ni njia yamlima Sekenke.
Haya ni mabaki ya mwili wa mmoja ya watu walikuwa kwenye lori hilo.
Moto ukimalizikia kwa mbali kama inavyoonekana