WALIO kitabilia chama cha mapiduzi (CCM) kifo na kukichongea
jeneza sasa wameanza kutapatapa kuzunguka nchinzima kunusuru chama chao.
Akizungumza
na wakazi wa jiji ni Mbeya katika maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM
yaliyofanyika jijini homo Rais Jakaya Kiwete alisema, walioitabilia Kifo CCM
sasa wanahangaika na kutapatapa kutafuta njia za kukunusuru chama chao.
Sasa
waliokitabilia mabaya chama hicho wanazunguka nchi nzima kutafuta mvuto kwa
wanachama wao na huku wakiwa na mgogogoro usio na msingi.
“Baadhi
yao sasa wanahangaika nchi nzima wakitapatapa kujinusuru wanakabiliwa na
migogoro mikubwa inayotishia uhai wao,” alisema Rais Kikwete.
Walijifanya
wao bundi na kukitabilia kifo chama na alisema kuwa wakati ule aliwaambia kuwa
CCM haita kufa na si ajabu wakafa wao badala ya chama hicho.
Alisema
kuwa kumekuwa na vyama vingi ambavyo vilisimama na kutikisa nchi lakini
unafiuka wakati vina dhohofika na kupoteza mvuto kwa jamii lakini CCM bado
inadunda.
Aidha
Rais alisema kuwa ni jambo la kitia moyo kuona CCM inaenelea kuwa chama kikubwa
na chenye nguvu kuliko vyama vyote hapa nchini mpaka kufikia miaka 37 tangu
kuasisiwa kwake.
“Wahenga
walisema dua la kuku halimpati mwewe na mchimba chimo hujifukia mwenyewe, na
CCM ipo hai na haina dalili ya ugonjwa wowote,” Aliongeza Rais.
Alisema
kuwa pamoja na chama hicho kuwa kikubwa na chenye nguvu lakini wasije wakalewa
sifa kufuatia mafanikio waliyo nayo na wakajisahau hata mara moja.
Aliongeza
kuwa kunahaja ya kuendelea kujiimarisha kwani wenzao wanaendelea kujiimarisha
kwa kiasi chao na kupata ,mafanikio kufuatia kujijenga kwao.
Rais
pia alizungumzia uchaguzi wa serikali za mitaa unaokaribia kufanyika mwaka huu
na uchaguzi mkuu kwa kuwataka viongozi wengine kuendelea kuimarisha chama ili
wapate mafanikio makubwa ilikupata ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa
kwani unamuhimu sana.
Furaha Eliab, Mbeya
LIKE ELIMTAA BLOG ON FACEBOOK HERE