Shinikizo dhidi ya Rais wa CAR


Watu wengi wameachwa bila makao kufuatia ghasia za kidini zinazoendelea nchini CAR
Viongozi wa kiafrika wanakutana hii leo kujadili ghasia za kidini zinazoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya kati .
Rais wake wa mpito Michel Djotodia, anatarajiwa kuhudhuria mazungumzo hayo yatakayofanyika katika nchi jirani ya Chad na waandishi wa habari wanasema huenda akakabiliwa na shinikizo la kumtaka aachie mamlaka baada ya kushindwa kusitisha ghasia hizo za kidini .
Waasi wa Seleka walifanya mapinduzi mwezi machi , na kumuweka mamlakani Djotodia kama rais wa kwanza wa kislam .
Rais aliyepinduliwa , Francois Bozize, ambaye anatoka katika jamii ya wakristo walio wengi alilazimika kwenda uhamishoni na taifa likajipatta katika limbo la ghasia . Zaidi ya watu elfu moja wameuawa katika kipindi cha mwezi mmoja pekee.
Afisa wa Umoja wa Mataifa ameiambia BBC kuwa mapigano katika taifa hilo yamewalazimisha watu nusu milioni kulundikana kataika kambi katika mji mkuu Bangui.
Na BBCSwahili