Sehemu
ya vijana wa UVCCM toka bara na visiwani wakitembea kutoka bandari ya
Dar es Salaam hadi makao makuu ya UVCCM katika kuadhimisha miaka 50 ya
mapinduzi ya Zanzibar huku na mabango yenye ujumbe mbalimbali wa
kuhamasisha Serikali mbili.(Picha zote na Zainul Mzige).
.awataka vijana kwenda kwa wananchi kuwaelimisha umuhimu wa Serikali mbili
.asema kero za Muungano zinaweza kupatiwa ufumbuzi
Na Damas Makangale, MOblog
MJUMBE
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo
Ndejembi amewataka vijana wa CCM kwenda kwa wananchi na kuwaelimisha
umuhimu wa kuwa na serikali mbili katika kulinda muungano wa Tanganyika
na Zanzibar.
Akizungumza
na wanamatembezi wa UVCCM kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya mapinduzi
ya Zanzibar leo mchana katika makao makuu UVCCM jijini Dar es Salaam ,
Ndugu Ndejembi amesema serikali mbili ndio nguzo kuu ya kudumisha
muungano kati ya bara na visiwani.
“tunataka
vijana waelewe kwamba serikali mbili ndio njia kuu ya kudumisha
muungano wetu kwa kuwa waasisi wa muungano Mzee Karume na Baba wa taifa
Nyerere walio mbali katika kuchanganya mchanga wan chi hizi mbili na
ndio njia bora katika kudumisha upendo, undugu na amani katika nchi
yetu,” amesema Ndugu Ndejembi.
Mjumbe
huyo wa NEC taifa alilisitiza kwamba mapendekezo ya tume ya mabadiliko
ya katiba ya serikali tatu itawagawa watanzania kati ya bara na visiwani
na ni serikali mbili ndio itawaleta karibu watanzania.
Ndejembi
aliongeza kuwa serikali tatu siyo suluhisho la kero mbalimbali za
muungano bali matatizo ya sasa ndani ya muungano yanaweza kushughulikiwa
na kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa maslahi mapana ya taifa.
Mjumbe
huyo wa NEC alisisitiza kwamba rasimu ya katiba ya pili iliyowasilishwa
hivi karibuni na Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Warioba katika
kipengele cha maadili na miiko ya uongozi, CCM haina matatizo kwa
maadili ya viongozi kuwekwa katika katiba kwa maslahi ya taifa.
Baadhi ya Wenyeviti wa UVCCM mkoa bara na visiwani mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya UVCCM jijini Dar.
Kwa
upande wake, Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Chief Sylvester
Yaredi aliyesoma risala ya wanamatembezi amesema takribani vijana 600
walishiriki matembezi hayo ambayo kati yao 35 walitoka katika maeneo
mbalimbali ya Tanzania Bara.
“tunaunga
mkono, kupongeza na kuenzi mapinduzi ya mwaka 1964, kwani mapinduzi
hayo ni alama ya ukombozi wa wanyonge waliokandamizwa, kuonewa na
kudhulumiwa haki na utu wao,” amesema Yaredi
Amesema
kuwa vijana wanatambua kuwa mapinduzi ya mwaka 1964 ndio chachu ya
muungano na kwamba vijana ndio tunu ya taifa na watalinda muungano kwa
nguvu zao zote.
Wanamatembezi wakiwa wamebeba picha za Waasisi wa Muungano na Viongozi wa sasa wa bara na visiwani.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea maandamano hayo.
Pichani
juu na chini ni MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC)
kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea picha za waasisi wa Taifa.
MJUMBE
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo
Ndejembi, akipokea picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo Ndejembi, akipokea picha ya Dkt. Ali Mohamed Shein Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Baadhi ya Wenyeviti wa UVCCM mikoani bara na visiwani wakiwa na bendera za Chama na Taifa.
Sehemu
ya vijana wakimsikiliza Mjumbe wa Halmashauri ya Taifa (NEC), Deo
Ndejembi, wakati akitoa hotuba fupi baada ya kupokea matembezi hayo ya
vijana.
Mjumbe
Baraza Kuu UVCCM Taifa, Chief Sylvester Yaredi, akisoma risala ya
vijana kwa Mjumbe wa NEC Taifa kupitia vijana Deo Ndejembi kuhusu
msimamo wa vijana wa serikali mbili katika kulinda muungano wa Bara na
Visiwani.
Mjumbe wa NEC Taifa kupitia vijana Deo Ndejembi, akimpongeza Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Taifa, Chief Sylvester Yaredi kwa risala nzuri.
MJUMBE
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo
Ndejembi, akizungumza na wanamatembezi kutoka UVCCM bara na visiwani
kuhusu umuhimu wa Vijana kutoa Elimu na kuhamasisha umuhimu wa Serikali
mbili kama njia bora ya kulinda Muungano wa Tanzania.
MJUMBE
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kupitia UVCCM, Deo
Ndejembi akisalimiana na baadhi ya vijana walishiriki matembezi ya
kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar waliowasili leo kutoka
visiwani Zanzibar.
Bi.
Hilda Oddy, Katibu kata ya Ubungo, Uhamasishaji (wa pili kulia) akiwa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wengine wa UVCCM.
Na MoBlog