SERIKALI KUREJESHA KIDOGOKIDOGO GHARAMA ZA EFD MASHINE


Mkuu wa wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya, Gurahamhusen Kifu

Mtoa Elimu wa mamlaka ya mapato Tanzania (TCRA) Kisa Kyejo
KUFUATIA kuwapo kwa maombi ya wafanyabiashara kuomba mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kutoa mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFD) bure na kukatwa kidogokidogo wakati wa kulipa kodi kitu ambacho hakiwezekani kwani mamlaka hiyo haifanyi biashara na kazi yake ni kukusanya kodi.
Hayo yamebainishwa na afisa wa elimu kwa mlipakodi wa (TRA), Kissa Kyejo katika mkutano wa wafanyabiashara wa Rujewa na mkuu wa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya mwishoni wa wiki iliyopita kufuatia kutolewa maoni mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara hao.
Alisema kuwa mamlaka haitaweza kuzitoa mashine hizo bure na kuwakata wananchi katika mapato yao kwani mamlaka hiyo haifanyibiashara na kuwakata wafanyabiashara wakati wa ukusanyaji wa mapato.
Kyejo alisema kuwa mamlaka hiyo si sawa na taasisi zingine za huduma kama shirika la umeme au mamlaka za maji ambazo zimekuwa zikitoa mashine bure na kuwakata wateja kidogokidogo gharama za mashine hizo.
Alisema kuwa mamlaka hiyo haiwezi kufanya biashara na hku ikikukusanya kodi na ndio maana ikatangaza tenda ya kuuza mashine hizo na watu wakashinda tenda za kufanya biashara hiyo.
Alisema kuwa mamlaka inafanya kazi ya kuwasimamia wauzaji na watengenezaji wa mashine hizo na kuhakikisha kuwa zinafanyakazi waliyoikusudia na kuwa mashine hizo zipo tafauti na zile zinazouzwa sehemu zingine kwa bei nafuu.
“Mashine hizi zipo tafauti na zile zinazouzwa Dubai na mashine hizi zinawasiliana moja kwa moja na TRA kwani hizo zingine hazina uwezo huo wa kutuma taarifa kwa mamlaka baada ya kufunga biashara kwa siku mashine hizi zinasifa zaidi ya 10 tofauti na hizo zingine,” Alisema Kyejo.
Afisa biashara wa mamlaka ya mji mdogo wa Rujewa
Alisema Serikali kwa kutambua umuhimu wa mashine hizo zitaingia nchini bila kutozwa kodi na kuingia nchini hasa ile kodi ya asilimia 80 kwani zikitozwa kodi ghalama itaenda kwa mwananchi moja kwa moja.
Kyejo aliongeza kuwa mfanyabiashara akinunua mashine hiyo gharama za ununuzi wa mashine hizo itarudi wakati wa kulipa kodi yake ile mfanyabiashara arudishiwe kidogo kidogo gharama ya ununuzi wa mashine hiyo.