Ulinzi mkali uliimarishwa mahakamani hapo |
MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imeahirisha kesi inayowakabili
Askali wawili na Raia watatu walioshitakiwa mahakamani hapo kwa kosa ya
ujambazi wa kutumia siraha baada ya msitakiwa mmoja kutofika mahakamani kwa
kisa cha kuwa anaumwa.
Kesi hiyo iliahilishwa na hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Hakimu
Michael Mteite baada ya kudaiwa kuwa Mshitakiwa wa tmbili kati ya watano Elinanzi
Mshana(22) anaumwa na kuwa hatofika mahakamani hapo.
Mteite alisema kuwa hata kwa machela mshitakiwa afike mahakamani
hapo ili awepo wakati kesi hiyo inasikilizwa na hicho sio kitu cha kuto fika mahakamani.
Alisema anaiahilisha kesi hiyo mpaka Januari 20 (Jumatatu) mwaka
huu na kuwa kesi itasikilizwa washitakiwa wote wakiwepo mahakamani.
Kutokana na hoja hiyo ndipo aliposimama Wakili wa Utetezi
ambaye anawasimamia washitakiwa wote watatu, Ladislaus Lwekaza na kuiambia
Mahakama kuwa Mshtakiwa namba mbili ameshindwa kuhudhuria kesi yake kutokana na
kuwa majeruhi yaliyotokana na kupigwa risasi sehemu ya paja hivyo kumfanya kuwa
na maumivu makali anayougulia akiwa gerezani.
Lwekaza alidai kuwa kutokana na mteja wake huyo kuwa
majeruhi aliiomba mahakama kuahirisha kesi hiyo hadi hapo mtuhumiwa huyo hali
yake itakapotengemaa na kuongeza kuwa pia hawataweza kuendelea na kesi kutokana
na washtakiwa wote kutopewa hati za mashtaka na maelezo ya mlalamikaji ili
wajiandae na utetezi.
Hata hivyo Wakili wa Serikali Mulisa alisimama na kumuuliza
Wakili wa utetezi kuwa anapaswa kuiambia mahakama kifungu alichotumia kudai
hati ya mashtaka pamoja na maelezo ya mlalamikaji sambamba na majeraha
aliyopata mtuhumiwa kuwa aliyapata wakati gani na lini.
Kwa upande wake Hakimu Mteite aliiambia Mahakama kuwa
kutokana na ubishani wa pande zote mbili ameona aingilie na kuwashauri kuwa
madai ya upande wa utetezi kuhusu hati ni haki ya kikatiba kupewa mshtakiwa.
Mteite aliongeza kuwa madai ya majeruhi ya Mshtakiwa namba
mbili ni mbinu za kuchelewesha kesi ambazo mara nyingi hufanyika ili mahakama
ishindwe kuendelea na kesi na kuongeza kuwa yeye binafsi pamoja na mahakama
hakubaliani na suala hilo.
Alisema kama taarifa za ugonjwa huo zingikuwa za kweli Jeshi
la Magereza linajua taratibu ambapo mgonjwa hupelekwa Hospitali ambapo mahakama
ikitambua huhamishia kesi zake hospitali.
Alisema Wakili wa utetezi anapaswa kutambua kuwa mwenendo wa
Mahakama wa siku hizo tofauti na zamani ambapo kesi moja ilikuwa ikichukua hadi
zaidi ya miaka mitatu lakini sasa wamejipanga kumaliza kesi mapema kabisa.
Kutokana na hali hiyo Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi
Januari 20 Mwaka huu na kumwagiza Wakili wa Utetezi Lwekaza kuhakikisha
inampeleka Mtuhumiwa siku ya kesi kwa njia yoyote hata kama ni mgonjwa namna
gani ikiwa ni pamoja na kumbeba kwa machela au gari la wagonjwa.
Pia alimwagiza mwendesha mashtaka wa Serikali kuhakikisha
anawapatia washtakiwa madai yao ambayo ni kupatiwa hati za mashtaka, nakala ya
maelezo ya mlalamikaji pamoja na mwenendo wa awali wa kesi.
Awali Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa
akisaidiwa na Basilius Namkambe alisema washtakiwa wote kwa pamoja
wanatuhumiwa kwa kosa moja la unyang’anyi wa kutumia Silaha kinyume cha Sheria
kifungu cha 287 sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Mulisa aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Mshitakiwa
namba moja ambaye ni Askari Polisi PC James mwenye namba F8302 wa Wilaya ya
Mbeya ambaye kabla ya kufikishwa mahakamani alivuliwa Uaskari baada ya
kuhukumiwa kijeshi.
Aliwataja wengine kuwa ni mshtakiwa namba mbili kuwa ni
Elinanzi Mshana(22)Mkazi wa Iyela Jijini Mbeya, Askari Magereza mwenye namba B
500 Sajenti Juma Mussa(37) wa Gereza la Ruanda Mbeya,Mbaruku Hamis(29) Mkazi wa
Iyela na Amri Kihenya(38) Mkazi wa Iyela.
Akisoma mashtaka yao Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama
hiyo, Michael Mteite, Mulisa alisema watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari
3, Mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mlima Kawetere barabara ya
Mbeya Chunya.
Alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo kwa
kulizuia gari aina ya Pick Up lililokuwa likiendeshwa na Ezekia Matatira (34)
Mkazi wa Iyunga Jijini Mbeya ambaye alikuwa na mtu aliyekuwa akifahamika kwa
jina la Sreedhar Pasupelet(38) mwenye asili ya Kiasia wakitumia magari madogo
mawili ambayo ni GX 100 Toyota Cresta T 782 BEU na Gari linguine ambalo
lilikuwa na namba za Chesesi GX 6011832 AINA YA Grand Mark II.
Na Mbeya yetu