AJALI Mbaya imetokea asubuhi hii na kudaiwa watu 10
kufa papo hapo na miili mingine kukwama ndani ya gari katika maeneo ya Ulyamtutu
barabara kuu ya Singida kuelekea Dodoma na Dar es Salaam gari mbili zimegongana
uso kwa uso ambapo Lori lemegongana na Noah.
Haijaweza
kufahamika gari hizo zilikuwa zikitokea wapi na kuelekea wapi kutokana na kuto
patikana mtu wa kiuzungumzia tukio hilo ambalo watu wote wamejeruhiwa.
Habari kutoka
katika eneo la tukio hilo zinasema kuwa sasa watu ndio wanajitokeza kutoa miili
iliyo nasa katika gari hizo.
Imedaiwa kuwa
gari aina ya Noah imeharibika vibaya na
kusambaratika kufuatia ajalihiyo ambayo im etokea katika maeneo ambayo sirahisi
kuamini kama imetokea ajali hiyo ukizingatia kuwa maeneo hayo hayana virima
wala vikwazo ambavyo vingeweza kusababisha ajali.
Imedaiwa kuwa dereva wa Lori amekimilia kusiko julikana bara baada ya tukio hilo kutokea.
Na Radio
Free Afrika Breaking News.