Rais Jakaya Kikwete akiwasili Viwanja vya Karimjee kuaga mwili wa marehemu Jaji George Bakari Liundi.
Rais Kikwete akiwa na Makamu wa Rais Dk. Gharib Bilal (kulia) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Wiliam Lukuvi (kushoto).
Wa kwanza kushoto (mbele) ni mke wa marehemu Jaji Liundi akiwa na wanafamilia wengine wakati wa kuaga.
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin Mkapa (katikati) akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kulia) na Salim Ahmed Salim (kushoto) nao walikuwepo kuaga mwili wa Jaji Liundi.
Mzee Mkapa (kati) akibadilishana mawazo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula (kulia).
...Mkapa akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia (kulia). Kushoto ni Pius Msekwa na Kinana.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, leo
ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Jaji George
Liundi katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Marehemu Liundi
ambaye alikuwa Msajili wa Kwanza wa Vyama vya Siasa nchini, alifariki
dunia Januari 12 mwaka huu alipokuwa akipelekwa Hospitali ya TMJ kwa
ajili ya matibabu. Marehemu Liundi amezikwa katika makaburi ya
Chang'ombe Maduka Mawili jijini Dar.
(PICHA NA HARUNI SANCHAWA / GPL)