AJALI YA SINGIDA VIFO VYAFIKIA 14




VIFO vimeongezeka katika ajali iliyo tokea jana mjini Singida na kufikia watu 14 kufuatia mmoja wa  majeruhi watatu kufa wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Itigi Singida.
Mtu huyo aliye fariki amefahamika kwa jina la Happiness Elisha mwenye umri wa miezi 6 amefariki usiku wa kuamkia leo.
Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea jana saa  1.32 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida. Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya kuja Singida mjini. Amesema hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia  maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida