MWENYEKITI
wa CCM Kata ya Kibamba, Ayoub Semvua akimpongeza Mbunge wa Temeke, Dar
es Salaam, Abbas Mtemvu, baada ya kuzungumza kama mgeni mwalikwa kwenye
Kichao cha kawaida cha Hamlashauri Kuu Kata ya Azimio jimboni humo,
jana jioni. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Kata hiyo Esa Uswege.
=================
BASHIR NKOROMO, TEMEKE, Tanzania
Mwenyekiti
wa CCM, Kata ya Kibamba, Dar es Salaam, Ayoub Semvua, amesifu kuwa kasi
ya utendaji kazi ya mbunge wa Temeke, Abas Mtemvu ni kubwa na huenda
inastahili kwendana na kasi ya utendaji wa Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itukadi na Uenezi Nape Nnauye.
"Nilipoitwa
na rafiki zangu hawa wa Azimio, sikujua kama na wewe utakuwepo, lakini
nikawa nimenuia kuwa hata kama hutakuwepo nitakusifia kwa kazi kubwa
unayofanya ya kimaendeleo katika kutekeleza ilani ya CCM katika jimbo
hili la Temeke... na sasa kuwa nimekukuta nitakusifu hapa hapa, wewe
kasi yako ya utekelezaji wa ilani ya CCM inatisha, na kwa kasi hii
unaweza kuwa unastahili kasi ya viongozi wetu Ndugu Kinana, Mzee
Mangula na Kijana wao Nape", alisema Semvua alipopewa fursa ya
kuzungumza kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, Kata ya Azimio,
ambacho alikuwa mgeni mwalikwa.
"Huyu
Katibu wetu Mkuu, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti Mzee Mangula na
kijana wao Nape, kasi yao ni kilometa 140 kwa saa. Kama kuna mtu
aliyeingia katika uongozi wa CCM kwa lengo tofauti kasi hii lazima
itamshinda na bora ajiondoe mwenyewe mapema", Semvua aliongeza.
Semvua
alisema, kutokana na utendaji bora na shirikishi wa Mtemvu, jimb\o la
Temeke limekuwa na sura tofauti kimaendeleo ikilingtanishwa na miaka 20
ikiongozwa na wabunge mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa sasa wa TLP,
Augustine Mtema ambaye amewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya
NCCR-Mageuzi.
"Mfano
mzuri wa maendeleo, niliyoshuhudia ambao kila mtu anauona ni barabara za
lami zilivyotanda katika maeneo mbalimbali ndani ya Temeke, tangu
nimetoka Kibamba nimeteleza kwa lami moja kwa moja bila kugusa udongo
hadi naingia kwenye Ofisi hii ya CCM Azimio", alisema Semvua.
Semvua
alisema, kutokana na kasi inayoonyeshwa na Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana na viongozi wengine kama Mtemvu, CCM itashinda urais
ba viti vingi vya ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa 2014.
Aliwataka
wana-CCM kuachana na tabia ya kuwa na nongwa aliyoifananisha na ya
kinywaji cha kahawa, ambayo baadhi wamekuwa wakidumu nayo kiasi cha
kuchagua wapinzani wakidhani wameikomoa CCM kumbe wamejikomoa wenyewe.
"Pale
wilaya ya Kinondoni tumepoteza viti viwili vya ubunge na vingi tu vya
udiwani na mitaa, sababu kubwa ni nongwa tu. Wanasema, Wakasema aaa,
bora tuupe upinzani tuheshimiane. Sasa ukiwauliza pale Kawe na Ubungo
kwamba mliwapa ubunge wapinzani sasa heshima gani mnapata? hawana jibu
zaidi ya kuinama chini", alisema Semvua.
Akifungua
kikao hicho, Mtemvu aliwataka wana-CCM na wananchi kwa jumla kuwapima
viongozi kwa utendaji kazi zao na sio kwa uhodari wa porojo nyingi kwa
sababu wananchi wanachohitaji ni maendeleo.
Alisema,
katika kipindi chake cha Ubunge, Temeke imeweza kuwa na barabara karibu
15 zenye lami hadi pembezoni mwa mji huo na kwamba zile zisizokuwa na
lami zimeboreshwa kwa kiwango kibwa kiasi cha kupitika nyakati zote.