MTOTO Getruda Krisantus wa miaka Mitatu mkazi wa kijiji cha Mkwajuni kata ya Mkwajuni wilayani Chunya Mkoani Mbeya amekufa maji katika dimbwai alilokuwa akiogelea.
Mtoto huyo alikufa maji juzi majira ya saa 12:00 jioni baada ya kuzidiwa na maji wakati akiwa na wenzake wakiogelea katika dimbwi la maji lililo karibu na mto Saza.
Akizungumzia tukio hilo kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Barakael Masaki alisema mtoto huyo alikufa baada ya kuzidiw ana maji.
Alisema kuwa mtoto huyo alikuwa akiogelea na wenzaka katika mto huo kabla ya kuzidiwa na maji.
Masaki alisema kuwa dimbwi alikofia maji mtoto huyo ni kubwa na liko karibu na maporomoko yam to Saza wilayani Chunya.
Alitoa wito kwa wazazi kwa kipindi hiki cha mvua kuwa makini na watoto wao na kuhakikisha wanawazuia kwenda kucheza katika madimbwi.
Hivyo ameitaka jamii kwa ujumla kuyafunika kwa miti mashimo yote yanayo weza kujaa maji katika kipindi hiki cha mvua ikiwa ni pamoja na visima vyote kuwekewa miti kwa juu ili kuepusha hatari za aina kama hii iliyo mkuta mtoto Getruda.
Alisema kwa kufanya hivyo tutawakinga watoto na majanga ya kufia katika maji katika kipindi hiki cha mvua.