WANANCHI wa mkoani Mbeya wametakiwa kuwa watunzaji wa amani kwa afya ya maendeleo yao na sio kwaajili ya wawekezaji pekee.
Akizungumza katika Hafla fupi ya kumuaga aliye kuwa Kamada
wa Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani na Kumkaribisha Kamanda mpya wa Polisi Mbeya
Ahmed Msangi, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kuwa uvurugaji wa
amani unavuruga utaratibu wa maendeleo.
Kuto kuwepo kwa amani kunasababisha wananchi kujichereweshea
maendeleo kwa sababu maduka yatafungu na kila huduma ya kijamii haita kuwa
ikifanya kazi.
Kama hakutakuw ana amani madhara si kukosa wawekezaji pekee
madhara ni kwa wakazi wenyewe kukosa wawekezaji ni madhala ya baadae.
“Kwa mfano wakazi wa Tunduma
wanajua madhara ya kuto kuwepo kwa amani kwa sababu hakuna kinacho weza
kufanyika kama kutakuwepo na uvunjifu wa amani,” Alisema Kandoro.
Kwa upande wake Aliyekuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya
Diwani Athumani alisema kuwa kuto kuwepo kwa vurugu mbalimbali kunasababisha
kurudi nyuma kimaendeleo.
Hivyo aliwaytaka wakazi wa jiji la Mbeya kushirikiana na
jeshi la polisi kuhakikisha amani inapatikana wakati wote jijini Mbeya.
“Mahali pasipo kuwa na amani wananchi wake wapo nyoma
kimaendeleo mdawote wanakuwa wapo katika mahangaiko na hawana mda wa kutulia
kufanya maendeleo ya aina yoyote,” Alisema DCP Athumani.
Nae Kamanda Msangi aliwataka wakazi wa jiji la Mbeya kutoa
ushirikiano kwa jeshi hilo ili kuhakikisha maendeleo ya amani yanakuwepo wakati
wote.