KITUO CHA POLISI OYSTERBAY KUBOMOLEWA NA KUJENGWA MADUKA YA KISASA.



 Kituo cha Polisi cha Oysterbay, pamoja na nyumba za Polisi wanaoishi katika Kambi hiyo, vitabomolewa kwa ajili ya kupisha ujenzi wa maduka ya kisasa mfano wa Mlimani City ujenzi unaotarajia kuanza mwakani.


 Tayari baadhi ya askari waliokuwa wakiishi katika Kambi hiyo wameshapewa 'Notis' ili kuhama katika nyumba zao na wengine kubomoa wenyewe majengo waliyokuwa wamejengwa kwa mabati katikati ya kambi hiyo ambayo walikuwa wakiishi, ambapo wengi wao waliokuwa wakiisha katika nyumba za mabati wamekwishabomoa nyumba zao na kuhama, huku baadhi wakiwa wamesalia wakisubiri awamu ya pili. Askari hao wameelekezwa kuhamia katika nyumba mpya zinazojengwa eneo la Kunduchi.
Baadhi ya askari wamelalamikia utaratibu huo wa kuhamishwa katika eneo hilo, hali ya kuwa pamoja na kubomolewa nyumba zao na Kituo cha Polisi, lakini imeelezwa kuwa kitajengwa Kituo kipya kikubwa katika eneo hilo ambacho kitajengea upande wa pili barabara ya Ubalozi wa Marekani.
Kinachowafanya baadhi ya askari kulalamikia utaratibu huo ni kutokana na kujengwa tena kituo kikubwa katika eneo hilo, lakini nyumba za askari zikiondolewa na kutotakiwa kuwepo tena, ambapo askari wote watapewa nyumba Kunduchi na kila atakayekuwa zamu atalazimika kusafiri ili kufika kazini, jambo ambalo limeonekana ni usumbufu na hasa pale itakapotokea dharula za kikazi.
Kamera ya Sufianimafoto, ilibahatika kukatiza katikati ya kambi hiyo na kushuhudia nyumba nyingi zikiwa tayari askari wameshahama huku zile za mabati zikiwa zimebolewa na askari wakiwa tayari wamehama huku wengine wakiendelea na zoezi la ubomoaji na kuhamisha mizigo yao kwa awamu.

HABARI ZAIDI BOFYA  http://www.sufianimafoto.com