SERIKALI ya Tanzania imelipongeza shirika la misaada la
Irish Aid kwa msaada wao walio utoa kwaajili ya kusaidia m aendeleo ya zao
kakao hapa nchini.
Hayo yalisemwa hivi karibuni wilayani Kyela na msahauri wa
kilimo mkoani Mbeya Chimagu Nyasebwa wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo ya
wawezeshaji wa shamba darasa la kakao, yaliyo andaliwa na shirika la
Technoserve wilayani Kyela hivi karibuni.
Mshauri huyo wa kilimo mkoani Mbeya alitoa kauli hiyo alipo
kuwa akiwahutubia wakulima na wawezeshaji wa mafunzo ya shamba darasa wapatao
60 waliohitimu mafunzo yao yaliyofanyika kwa wiki mbili wilayani Kyela
Wahitimu 60 wamafunzo hayo walitoka katika wilaya nne za
mikoa tofauti hapa nchini ambazo ni Kilombelo (7), Rungwe (21), Kyela (32) pamoja
na mshiriki mmoja kutoka katika wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Nyasebwa ambaye pia alikuwa mgeni Rasmi katika sherehe hizo
alisema Serikali inatambua umuhimu wa zao hili, na jitihada zaidi zinafanywa
ili kuweza kuliboresha.
Alisema mafunzo ya wiki mbili ambayo wakulima 60 wamepatiwa
kutoka kwa wasimamizi wa mafunzo wa shirika la Technoserve ni ya muhimu zidi,
hivyo watu hao wanastahili kupongezwa kwa kazi nzuri waliyo ifanya.
Mshauri huyo wa kilimo wa mkoa Mbeya aliongeza kuwa wakulima
wanapaswa kujifunza mbinu za uzalishaji kwa pamoja, ili waweze kuongeza kipato
chao na kuzingatia mafunzo waliyo yapata ili yaweze kunufaisha sekta ya kilimo.
Kiongozi huyo wa kilimo alisema katika mradi huo unaolinga
kuboresha kilimo cha kakao hapa nchini, wakulima 18 wameweza kufikia kiwango
cha asilimia 42.
Alisema kwa wakati huu zao la kilimo cha kokoa linazidi
kukua na kuongeza uchumia wa taifa, hivyo mikakati ya huboresha zao hili
inafanywa ili iweze kuzaa matunda.
Alisema, mikutano ya kukaa na wadau itasaidia kujadili
changamoto zinazo wakabili wakulima, na serikali itahakikisha kwamba inasimamia
kikamilifu katika kuleta uboreshaji.
Nyasebwa aliwaambia wahitimu hao wa shamba darasa la kilimo
kuwa serikali pia inasisitiza ushiriki wa vijana, katika sekta kilimo ili
kuboresha nguvu kazi, na kwamba serikali
itahakikisha inasimamia miradi yote inayo letwa na wafadhili ili isipotee bure.
Meneja wa mradi huo wa Technoserve Joseph Mabura alisema
wahitimu wamejifunza mbinu mbalimbali za uzalishaji pamoja na usindikaji wa
kakao.
Alisema kuwa mradi huo unauwezo wa kuwafikia wakulima
wapatao 18,000 kwa kipindi cha miaka 10 ijayo, hivyo ni muhimu kwa wawezeshaji
kujifunza pia mambo ya kijamii kama vile Ukimwi.
Mabula alisema kuwa
mradi huu wa kokoa ulipoanzishwa wilayani Kyela na sehemu nyingine hapa
nchini kumekuwepo na maendeleo makubwa .
Nae afisa kilimo umwagiliaji na ushirika wilayani Kyela
Joseph Nyau alisema kuwa wilaya zinazo lima zao la kokoa hapa nchini zinazidi
kuongezeka, na kuzitaja kuwa ni Mtwala, Lindi, Morogoro katika wilaya ya
Kilombelo, Kyela, pamoja na wilaya mpya ya Nyasa kukota mkoa wa Ruvuma.
Mpaka sasa Kyela kunawatumishi wapatao 48 wanao toa mafunzo
ya kilimo shamba darasa, na kwamba wilaya hiyo ndiyo inayoongoza kwa uzalishaji
wa zao kokoa hapa nchini.
Aidha kiongozi huyo alisema kuwa wakati shirika la
Technoserve wanaingia wilayani Kyela beo ya kokoa kwa kilo moja ilikuwa ni kati
ya shilingi 1,500-1,800,lakini kwa sasa kokoa inauzwa kwa shilingi 3,000 kwa
kilo.
Na George Chanda