Cameron aongoza wafanyabiashara China


Waziri Mkuu David Cameron awasili China

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amemwaambia waziri mkuu wa China, Li Keqiang, kuwa anapendelea kuona mkataba wa biashara huria unafanyika kati ya Umoja wa Ulaya na China.

Bwana Cameron anaoongoza ujumbe mkubwa wa wafanyabiashara wa Uingereza unaozuru China-- ikiashiria kumalizika kwa uhasama wa kimawasiliano kati ya viongozi wa ngazi ya juu wa nchi mbili hizo.
Hali hiyo inatokana na hatua ya waziri mkuu Cameron kukutana mwaka jana na kiongozi wa kiroho kutoka Tibet, nchini China, Dalai Lam ambaye anaishi uhamishoni. Siku ya Jumatatu, Bwana Cameron alishuhudia kutiwa saini kwa mikataba mbalimbali ya kibishara.

Hajatamka lolote hadharani kuhusu rekodi ya ukiukaji wa haki za binadamu au mgogoro kuhusu jimbo la Tibet nchini China.

Wanaharakati wamemshutumu Bwana Cameron kwa kuonekana mfanyabiashara zaidi kuliko kuwa kiongozi.

Miongoni mwa waliofuatana na Bwana Cameron katika ziara nchini China, mkuu wa kampuni ya kutengeneza dawa ya GlaxoSmithKline, ambayo mauzo yake nchini China yameathiriwa vibaya na kashfa ya rushwa katika biashara zake.
Na bbc