Ofisi ya bajaj Mbeya
Bajaj zikiwa zime paki
Madereva wa Bajaj Mbeya
- WATUMIAJI WALALAMIKA
MADEREVA wa Bajaj Jijini Mbeya wamesitisha kutoa huduma ya
usafiri kwa muda wa masaa 5 wakishinikiza uongozi wa chama cha Waendesha Bajaj
kuzirejesha pesa zinazo daiwa kutafunwa.
Madereva hao walifikia uamuzi huo kufuatia viongozi wa chama
hicho kuzitafuna pesa zao zinazotokana
na michango yao mbalimbali baada ya kuhoji matumizi ya pesa hizo.
Ubadhilifu huo umegundulika juzi baada ya kudai kusomewa
mapato na matumizi ya pesa ambazo wamechanga kwa takribani mwaka mzima.
Mmoja wa wafuatiliaji wa kalibu na kiongozi wa nidhamu
barabarani kwa madereva hao, Twaha Ramadhani, ambaye pia jana alipelekwa
mahabusu kwa tuhuma za kusababisha uvunjifu wa amani alisema kuwa viongozi hao
wametumia pesa nyingi za michango yao.
Alisema kuwa yeye kuna kipindi alipewa kukusanya pesa za
chama hicho ambazo zilifika zaidi ya laki 6 lakini wakati wanasomewa mapato
waliambiwa pesa zilizo kusanywa ni laki 1.8 ambazo zimekusanywa.
Alisema mbali na pesa hizo alizozikusanya pia wana miradi mingi
ambayo imekuwa ikiwaingizia pesa lakini hawajaziona katika mapato yao ya mwaka.
Ramadhani kufuatia
ufuatiliaji wake huo wa pesa za chama hicho alikamatwa na Polisi usiku wa jana
akidaiwa kuvuruga amani, kitu anacho sema si sahii na tuhuma hizo zilitengenewa
na uongozi unao tuhumiwa na chama hicho.
“Mimi wamenikamata usiku wa leo wakinituhumu kuhusika na uvunjifu wa amani walikuja Askali sita usiku wa saa 8 walinikuta nimelala na wakanichukua baada ya kuwauliza walicho nikamatia walisema kuwa nahusika kufunga ofisi na kuchana bendrea ya taifa kitu ambacho mimi sijahusika na ufungaji wa ofisi na kuchukua bendera,” Alisema Ramadhan.
Aliongeza kuwa walipo mfikisha mahabusu walio mtuhumu
wakaonekana wametengeneza tuhuma na kumuachia huru.
Madereva hao mbali ya kuwatuhumu viongozi hao pia waliamua
kusitisha huduma kufuatia kukamatwa kwa Ramadhan ambapo baada ya kurudi kwake
wakaenderea kutoa huduma.
Kwa upande wake mkuu wa vituo vya Matraf mkoani Mbeya,
Kevini Ndimbo alisema kuwa vyama vinapoazisha wahakikise kuwa wanakuwa na
akaunti za benki ili kuwa na usalama wa pesa zao ambazo zimekuwa zikitunza
mikononi mwa viongozi.
Alisema kuwa kuwapo kwa akaunti za benki kutasaidia uwepo wa
usalama wa pesa za wanachama vya vyama hivyo.
Alivishauri vyama
hivyo vinapo anzishwa ni vyema kuwashirikisha wanasheria ili kuweka chama chao
kuwa kisheria na kulinda haki zao.
Kwa upande wa watumiaji wa usafili huo wa bajaj wamesema
kuwa watoa huduma hao ni muhimu kwani wamepata shida kusitishwa kwa huduma hiyo
kwa muda huo mfupi.
Mmoja wa watumiaji wa huduma hizo Sifael Kyonjola alisema
kuwa kwa muda mfupi huduma zilivyo sitishwa wamepata shida na kuwafanya kucherewa
katika shuguli zao mbalimbali za kila siku.