AFA KWA KUGONGWA NA GARI



MKAZI wa Katumba wilayani Rungwe Mkoani Mbeya Amoni Abilia (22) amekufa baada ya kugongwa na gari katika maeneo ya Katumba wilayani Rungwe.

Ajali hiyo ilitoikea juzi katika maeneo ya Katumba barabara ya Tukuyu /Mbeya ambapo dereva wa gari iliyo sababisha ajali ilitokomea kusiko julikana.

Kimu kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya Barakaeli Masaki alisema kuwa ajali hiyo chanzo chake kinachunguzwa.

Alisema gari ambayo ilisababisha ajali hiyo ilitokomea kusiko julikana mara baada ya kusababisha ajali hiyo.

Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika hospitali Makandana wilayani Rungwe.

Alisema marehemu aligongwa na gari wakati akijaribu kuvuka barabara katika maeneo ya Katumba.

Barakael amewataka wananchi kuwa makini wakati wakivuka barabara kwa kipindi hiki cha sikukuu.