Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahmna Kinana akishiriki ujenzi wa msingi ya wodi y a
wazazi ya kituo cha afya kata ya Lubanda wilayani Ileje.
Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akishirikiana na
wananchi wa kata ya Lubanda kujenga msingi wa wodi ya akina mama katika
kituo cha afya cha kata hiyo wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwa nyumbani kwa Balozi wa Shina namba 1
Balozi Nosadi Edward (mwenye fulana kulia),Katibu Mkuu amekuwa na
utamaduni wa kutembelea mabalozi katika ziara zake .
Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akisalimiana na
wakazi wa shina namba 1 kata ya Sange ,wilaya ya Ileje mkoan Mbeya.
Wasanii wa ngoma
wakicheza ngoma ya Ibandi ngoma maarufu ya kabila la Wandari wakati wa
kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana Ujumbe wake
ambao walitembelea kata ya Kalembo ,wilaya ya Ileje mkoani Mbeya.
Diwani wa Kata
ya Isongole Ndugu Gwalusako Kapesa akielezea namna gani wananchi wa
ilaya ya Ileje wamechoshwa na taratibu za serikali za kuwalazimisha
kununua mbolea za ruzuku za Minjingu kwani zimekuwa hazina faida kwao
kama wakulima na zimewaletea hasara kubwa sana, wananchi hao wameiomba
serikali na viongozi wake kuwasikiliza zaidi wao katika kutatua kero
zao.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya
Kalembo na kuwaambia kilio cha wakulima kinafanana karibia nchi nzima
hasa kuhusu matatizo ya mbolea na kusema CCM itachukua hatua kwa
kukutana na waziri husika kwenye kamati kuu itakayofanyika mapema mwezi
ujao.
Wananchi wa Kata
ya Kalembo wakiwa wamejifunika miamvuli kujikinga na mvua wakati wa
mkutano na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake
ambao upo ziarani mkoani Mbeya.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za kumbukumbu za kifo cha
marehemu Steven Kibona kwa wananchi wa kata ya Kalembo, kushoto ni mjane
wa marehemu Mama Kibona.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya
ya Ileje Ndugu Rosemary Sinyamule kwenye daraja la mto Songwe mpakani
mwa Tanzania na Malawi,Mkuu wa Wilaya alimueleza Katibu Mkuu kuwa kuna
eneo hilo lina fursa nyingi kibiashara na kiuchumi kama barabara ya
lami itajengwa na ikiwa pamoja na ofisi za kudumu za uhamiaji
zitajengwa katika kata ya Isongole.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa
Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro wakizungumza na wananchi wa
kata ya Isongole wilaya ya Ileje mpakani mwa Tanzania na Malawi.
Katibu Mkuu wa
CCM akiwa nje ya ofisi ya uhamiaji ya kata ya Isongile wilaya ya Ileje
mkoani Mbeya,kushoto ni mkuu wa kituo hicho cha uhamiaji Ndugu Fredrick
Luhanga
Na Mkonowangu Blog