Valdis Dombrovskis,waziri mkuu wa Latvia |
Waziri Mkuu wa wa Latvia, Valdis
Dombrovskis, amejiuzulu kufuatia kuporomoka kwa jengo moja nchini humo,
Alhamisi iliyopita na kusababisha watu wapatao hamsini kuuawa.
Bwana Dombrovskis amesema amekubali kuwajibika
kisiasa kutokana na mkasa huo ambapo paa ya duka moja kubwa la bidhaa
katika mji mkuu, Riga, lilipinda na kuporomoka.Polisi wameanzisha uchunguzi wa kihalifu kubaini kama taratibu za ujenzi wa jengo hilo zilizingatiwa au la; bustani ilikuwa ikijengwa juu ya paa la jengo hilo la maduka wakati ajali hiyo ikitokea.
Latvia imekuwa na siku tatu za maombolezo kuwakumbuka waathirika wa janga hilo, ambalo ni baya kuwahi kutokea nchini Latvia, tangu nchi hiyo ijipatie uhuru wake mwaka 1981.
Kujiuzulu kwa Bwana Dombrovskis, ambaye ameiongoza Latvia katika kipindi cha mgogoro wa kiuchumi, kumekuja wiki kadhaa kabla ya nchi hiyo kujiunga na umoja wa Ulaya.