Watu wasiopungua 100 wanahofiwa wamekufa kwenye mvua kubwa inayoshesha
katika eneo la Puntland kaskazini mwa Somalia. Hayo yamesemwa na
serikali ya jimbo la Puntland
Habari zilizokusanywa kutoka maeneo ya pwani kupitia mawasiliano ya kawaida ya simu katika kipindi cha saa 48 zilizopita, zinaonyesha kuwa hadi watu 100 huenda wameuawa , wakati mamia ya watu wengine hawajulikani waliko.
Rais wa eneo linalojitawala la Puntland Abdirahman Mohamed Farole amesema "mzozo huo ni mkubwa" huku serikali ikitangaza hali hiyo kuwa ni janga.
Serikali inaendelea na shughuli za kusambaza misaada ya dharura kwa walioathirika, lakini pia imetoa wito kwa jamii ya kimataifa kutoa mchango wao. Mvua kubwa pamoja na upepo mkali unatarajiwa kuendelea kulikumba eneo hilo hadi Jumatano wiki hii.
Habari na DW.DE