Viongozi wa Jubilee nchini Kenya, wameyakosoa mataifa ya Magharibi kwa
kuisaliti Kenya na kwamba yamechangia kushindwa kwa hatua ya Umoja wa
Afrika ya kulitaka Baraza la Usalama, kuahirisha kesi ya Kenyatta na
Ruto.
Viongozi hao wanashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika
Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC, The Hague. Grace Kabogo
amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya, Barack Muluka
na kwanza alitaka kujua Jubilee wametumia misingi gani kuzilaumu nchi
hizo? Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo
chini.