Ni Picha za wiki hii nilizotumia na mdau Kanuth zikionyesha baadhi ya
maeneo ya Mto Rufiji kwenye kijiji cha Mloka huko Rufiji. Sina haja ya
kusema maneno mengi lakini kwa hali inayoonekana ni dhahiri hali ya kina
cha maji kwenye mto huu imefikia kina cha chini mno. Huu ni mto ambao
wageni huwa wanatembezwa kwa maboti kwenye zile boat safaris. Sasa hivi
hata hizo boat safaris zinafanywa kwa nadra na kwenye eneo dogo. Wageni
wanalazimika kutembea kuifuata boat mahali ambapo kina cha maji
kinaiwezesha kuanza safari. Sehemu ambazo majani yameota ni sehemu
ambazo kwa kawaida huwa zimefunikwa na Maji kipindi ambacho si cha
kiangazi. Kukupa picha ilivyo, naomba urudie posts hizi kadhaa za mto
huu ambazo zinaonyesha hali inavyokuwa kipindi kingine cha mwaka.
Kwa kawaida hapa maji huwa yanakuwa yamejaa mwanzo mwisho. sasa hivi ni visiwa vya mchanga na majani
Hapo inatafutwa sehemu ya kuegeshea boat ili wageni waweze kupanda na
kuanza boat safari. kwa kipindi cha kawaida eneo hili huwezi kulifikia
kwa kutembea kwa miguu.
Shukran ya picha kwa Mdau Kanuth wa Kanuth Adventures