Mwanaume wa Somalia akamatwa kuhusiana na kuteketea kwa meli ya wakimbizi pwani ya Italia
Mwanaume huyo, aliyetajwa jina na polisi kama Elmi Mouhamud Muhidin,
alikamatwa katika kisiwa cha Lampedusa ambako alikuwa akiishi katika
kituo cha wahamiaji kilichojaa sana na kujidai kuwa mmoja wa wakimbizi.
Wachunguzi walisema baadhi ya waliopona katika balaa hilo walimuona katika kituo na kumtambua kama mwanachama wa viongozi wanaofanya biashara ya magendo ya wahamiaji kutoka Libya kwenda Italia.
Kwa pamoja na baadhi ya wapiganaji wa Libya, mtu huyo pia anashutumiwa kwa kuhusika katika ubakaji wakati wahamiaji wanaposhikiliwa katika kituo cha kuzuia wakimbizi katika jangwa la Libya.
Kapteni wa boti wa Tunisia, Khaled Bensalam, alikamatwa mara moja baada ya janga hilo kwa mashitaka ya mauaji ya watu.
Kuteketea kwa meli kuliua wahamiaji 366, wengi kutoka Eritrea na Somalia, baada ya boti kuwaka moto na kupinduka karibu na ufukwo wa kisiwa cha Italia cha Lampedusa tarehe 3 Oktoba.