Mazungumzo magumu yanaanza leo kati ya Iran na mataifa makubwa kutafuta
makubaliano kwa mpango wa nyuklia wa Iran ambayo pia yatawaridhisha
wanasiasa wa msimamo mkali huko Marekani, Israel na Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran.
Israel imekanusha madai hayo na Waziri Mkuu wake Benjamin Netanyahu leo hii anatarajiwa kuendeleza kampeni yake dhidi ya kufikia makubaliano ya nyuklia na Iran wakati atakapokutana na Rais Vladimir Putin wa Urusi mjini Moscow.
Iran ina matumaini
Iran Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif ameonekana kutokata tamaa kuhusu nafasi za kufikiwa kwa makubaliano mjini Geneva ikiwa ni siku 10 baada ya mazungumzo kati ya Iran kwa upande mmoja na kwa upande wa pili Marekani, China, Urusi, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kushindwa kufikia makubaliano.Amekaririwa akisema kwamba anadhani kuna kila uwezekano wa mafanikio.
Rais Barack Obama wa Marekani. |
Wabunge wa Marekani hapo jana wameitaka serikali ya Marekani iwe na msimamo mkali katika mazungumzo yake na Iran kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi hiyo.
Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ilisema jana kwamba waziri mkuu huyo pia alizungumza kwa simu na Rais Hassan Rouhani wa Iran ambayo yalikuwa ni mawasiliano ya kwanza kati ya viongozi wa nchi hiyo katika kipindi cha muongo mzima na viongozi hao wamekubali kwamba ni muhimu kuitumia fursa iliopo.
Vitisho na vikwazo vikomeshwe
Rais Hassan Rouhani wa Iran. |
Mataifa makubwa yanataka kufikiwa kwa makubaliano ya awamu ya kwanza ambapo kwayo Iran inatakiwa isitishe sehemu ya shughuli zake nyeti kabisa za nyuklia wakati makubaliano ya muda mrefu yakiandaliwa.Lakini suala ni iwapo Iran yenye kupigania kuregezwa kwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa,Marekani na Umoja wa Ulaya ambavyo vimeathiri sana usafirishaji nje wa mafuta ya nchi hiyo itakubali kile kinachopendekezwa badala yake.
Wataalamu wanasema iwapo haiba ya uchangamfu anayoitumia Rais Rouhani kuwasiliana na mataifa ya magharibi itashindwa kuupatia ufumbuzi mzozo wa nyuklia wa nchi hiyo atakuwa katika hatari ya kuacha kuungwa mkono na kiongozi mkuu wa nchi hiyo Ali Khamenei ambaye leo amesema mataifa ya magharibi lazima yaheshimu mistari mekundu ya nchi hiyo na pia kuitaka serikali ya Iran kuheshimu mistari hiyo na kutotiwa kiherehere na makelele ya maadui na wale walioko dhidi ya Iran.