Bashar al-Assad hatahudhuria mazungumzo

Mazungumzo  ya  amani  ya  Syria  ambayo   yatafanyika Januari  mwakani  yatafanyika  bila  ya  kuwapo  rais Bashar al-Assad  ama  makundi  yenye  msimamo  mkali. 

 Waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Ufaransa  Laurent Fabius  amesema  leo, lengo  la  mkutano  wa  Geneva II, si  la  gumzo  kuhusu  Syria , badala  yake  ni  la kufikia makubaliano  ya  pande  zote  kati  ya  wawakilishi  wa serikali  ya  rais Assad  na  wapinzani  wenye  msimamo wa  wastani  ili kuunda  serikali  ya  mpito.
Fabius  amesema  hayo  siku  moja  baada  ya  Marekani na  Urusi  kuweka  uzito  katika  mazungumzo  hayo yaliyocheleweshwa  kwa  muda  mrefu, ambayo  Umoja  wa Mataifa  umesema  hatimaye  yatafanyika  Januari 22. 
Mpatanishi  wa  kimataifa  nchini  Syria  Lakhdar Brahimi amesema  orodha  ya  washiriki  haijapangwa. 
Msemaji  wa wizara  ya  mambo  ya  kigeni  Romain Nadal  amesema Ufaransa  inataka  pande  zote  kutuma  ujumbe  mmoja kila  mmoja.
Habari na DW.DE